Taarifa Mbaya Kutoka Simba Kuhusu Kuvunjika Kwa Ivo Mapunda


Wakati zikiwa zimebakia takribani wiki mbili kabla ya kukutana na mahasimu wao wa jadi, klabu ya Simba imepata pigo kubwa katika timu.
Kipa namba moja wa timu hiyo, Ivo Philip Mapunda amevunjika kidole mazoezini Zanzibar jaa asubuhi na anatakiwa kuwa nje kwa wiki nane- maana yake hataweza kusimama langoni timu hiyo ikimenyana na watani, Yanga SC Oktoba 12.
Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amesema kwamba, Ivo aliumia wakati anachupia mpira katika mazoezi ya asubuhi na kwa bahati mbaya mpira ukamgonga kwenye kidole kidogo cha mwisho mkono wa kulia.
Gembe amesema Ivo alitoka mazoezini baada ya tukio hilo na baadaye akapelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kisiwani humo, ambako baada ya vipimo ikagundulika amevunjika sana. “Si kuvunjika kwa mzaha, amevunjika sana na anatakiwa kupumzika kwa wiki nane, baada ya hapo aanze taratibu, ina maana makadirio ya kurudi tena uwanjani ni hadi baada ya miezi mitatu,”amesema Gembe.
Kuumia kwa Ivo kunatoa nafasi kwa makipa chipukizi, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ na Peter Manyika kujibidiisha ili kuziba pengo lake.
Ivo anafanya idadi ya wachezaji wanne tegemeo majeruhi Simba SC, baada ya Paul Kiongera anayetakiwa kuwa nje wiki sita, Haroun Chanongo na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ ambao hawatahitaji zaidi ya wiki ya moja ya kuwa nje ya UwanJa

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini