ESCROW:Majibu ya PROF MUHONGO ni Aibu ya Mwaka kwa PAC na Wasaka Tonge

 
Kwa aliyefatilia majibu ya waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo leo bungeni akijibu hoja za kamati ya PAC atakubali kuwa kamati ya ZITTO KABWE imewadanganya watanzania. Muhongo ambaye amejibu hoja moja baada ya nyingine kwa kutoa ushahidi wa viambatanisho muhimu amedhihirishia bunge kuwa kamati ya bunge imetoa taarifa ya uongo. 

Katika majibu yake, profesa Muhongo amedhihirisha kwa ushahidi kuwa pesa za ESCROW hazikua za serikali. Pesa hizo ni za IPTL na kwamba serikali bado inadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 94 na IPTL kama malipo ya kufua umeme. 
Aidha, Muhongo amemlipua mwanasheria Mkono ambaye aliingia mkataba na TANESCO wa kuwa mwanasheria wao na alidai na kulipwa kiasi cha bilioni 62 (robo ya pesa za ESCROW) kama malipo ya uanasheria. Mkataba huu ulivunjwa na TANESCO chini ya uongozi wa waziri Muhongo. 

Majibu haya ya Muhongo yameivua nguo kamati ya PAC na kuzua maswali mengi yasiyo na majibu. 
Kwanini PAC ilidanganya bunge? 
Kwanini PAC haikuonesha vielelezo hivyo? 
Nani yako nyuma ya PAC? 
Kwanini PAC haikutaja ufisadi huu wa Mkono? 
Taarifa kuwa wasaka Urais wa CCM ndio waliopika uongo huu tuziamini?

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini