SUALA LA KUHUSISHA TOHARA YA WANAUME NA IMANI ZA DINI LAKEMEWA VIKALI MKOANI NJOMBE

 
Na Eddy Blog, Njombe
Wananchi mkoani Njombe wameaswa kutoliingiza suala la tohara ya wanaume na imani za dini kwa kuwa suala hilo ni kwa ajili ya kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na manufaa mengine ya kiafya na si vinginevyo

Hayo yamebainika wakati wa uchangiaji mada iliyowasilishwa katika kikao cha wadau wa mapambano dhidi ya vvu kilichoandaliwa na tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) ambapo imeonekana miongoni mwa changamoto ambayo shirika la JHPIEGO lilikutana nayo wakati wa utekelezaji wa huduma ya tohara ya wanaume ni imani ya dini

Mmoja wa wachangiaji hao askofu mstaafu Dkt Peter Lukumbusho Mwamasika ameeleza kuwa wapo baadhi ya watu wanadai wanaume wakifanyiwa tohara wanakuwa wamehamishwa katika imani yao ya kikristo na kupelekwa katika imani ya kiislamu jambo ambalo limepingwa vikali kuwa halina ukweli wowote
Askofu huyo amesema katika kipindi hiki ambacho kila mmoja anapambana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, tohara imegundulika kuwa ni moja ya njia inayopunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa waliofanyiwa tohara hivyo mwanaume aliyefanyiwa tohara imani yake ya dini inabakia pale pale
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayoshughulikia Ukimwi Mh. Lediana Mng'ong'o amewataka viongozi wa siasa kushirikishwa katika jitihada za kupambana na maambukizi ya VVU
"Humu ndani siwaoni madiwani, siwaoni wenyeviti wa halmashauri, angalau nawaona wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri ndio wasimamizi wa sheria ndogondogo ninaomba tuwashirikishe sana maana wanaushawishi mkubwa katika hili" amesema Mng'ong'o
Amesema kwa nafasi hii wakishirikishwa viongozi wa siasa watakuwa wanapeleka taarifa hizo kwa wapiga kura wao suala hilo litasaidia kuwa na mabadiliko makubwa katika jamii  

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini