Tangazo la msiba wa Kepteni Kaluse aliyefariki katika ajali ya helkopta Dar


Mrakibu wa Polisi-Captain Kidai Senzala Kaluse enzi za uhai wake. 
Familia ya Mzee Senzala Kaluse wa Kimara Mwisho Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao KIDAI SENZALA KALUSE kilichotokea Novemba 29, 2014 Saa 4 asubuhi kwa ajali ya ndege aina ya helkopta huko Kipunguni B, Moshi Bar, Dar es Salaam.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa baba yake Mzee Kaluse huko Kimara Mwisho.
Habari ziwafikie, Ukoo wote wa Warutu, Ukoo wa Kaluse, Ukoo wa Mroki, Familia yote ya Timothy Nathan, Ukoo wa Kajiru na Taluka, Wakamba wote wa Ugweno Msangeni, Bibi wa Marehemu Mary Nathan wa Kinyenze- Morogoro, Familia ya Tarimo ya Ukonga Mombasa, Omary Msuya wa Moshi, Abdalh Mgonja wa Gonja Maore, Hosea wa Arusha.

Taarifa pia ziwafike maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Kikosi cha Polisi Anga, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

Misa ya kuaga Mwili wa Marehemu itafanyika mnyumbani kwao kuanzia Saa 6:00 kabla ya safari ya kuelekea Gonja Maore, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kuanza na mazishi yatafanyika Jumatatu Kijijini Kwao Gonja Maore.

Mawasiliano zaidi: Mroki Mroki- +255 717002303. 

MATAYO 5: 4 HERI WENYE HUZUNI; MAANA WAO WATAFARIJIKA



TAARIFA

Marubani watatu wa polisi pamoja na rubani mmoja wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliyetambuliwa kwa jina la Joseph Alfayo wamekufa baada ya helkopta waliyoruka nayo katika ukaguzi wa kawaida kuanguka.

Helkopta hiyo namba 5H- TWA ni mali ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Ajali hiyo imetokea leo saa 4 asubuhi maeneo ya Ukonga Moshi Bar.

Akizungumza katika eneo la tukio, Kamanda wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kamishna Suleiman Kova alisema, chanzo cha helkopta hiyo kuanguka bado hakijajulikana na uchunguzi kujua chanzo unaendelea.

Aliwataja wengine waliokufa ukiachia Alfayo kuwa ni Mrakibu wa Polisi Kapteni Gidai Sindano, Mkaguzi wa Polisi Inspekta Simba Muta na askari PC Josu Selisina.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini