Picha: Wasanii wa Marekani walivyosherehekea siku ya Halloween


Beyonce akimbusu mwanae kipenzi Blue Ivy aliyevalishwa kama Billie Jean.


Billie Jean mwenyewe Michael Jackson wakati wa uhai wake.


North West ambaye ni mtoto wa Kanye West akiwa amevalishwa mtindo wa kipekee katika sikukuu hiyo.



Mariah Carey akiwa na wanae mapacha.


Mkali wa “I was born to make you happy” akifurahia na watoto wake pamoja na mama yake.


Kim Kardashian akiwa na mwanae pamoja na rafiki yake.


Jay Z alitoka na binti yake Blue Ivy ambae alivalishwa kama Billie Jean wa Michael Jackson.
Nyota wengi wa sanaa ya filamu na muziki nchini Marekani wakiwa na familia zao wamesherehekea siku ya Halloween kwa kuvaa mavazi ya ajabu, kutisha, kuvutia na mengine yenye kupendeza.
Jay Z na mkewe Beyonce walimvalisha mtoto wao Blue Ivy kama Billie Jean, moja ya nyimbo aliyowahi kuimba gwiji wa Pop Michael Jackson, mtoto wa Kanye, North West naye alivalishwa nguo za ajabu na zenye kuvutia huku mama yake Kim Kardshian akiwa amevaa nguo yenye picha fuvu la binadamu.
Hivi ndivyo baadhi ya mastaa walivyosherehekea siku hiyo inayoadhimishwa Oktoba 31 kila mwaka.


Halloween ni sherehe ya kila mwaka ambayo hufanyika katika mataifa kadhaa kila Oktoba 31, ambayo ni siku kabla ya kufunga kwa Wakristo wa Magharibi kwa siku zote za Hallow.
Ni wakati ambao watu hukumbuka wafu, wakiwemo watakatifu (hallows), watu waliouawa bila hatia,  na watu wenye imani waliotangulia.
Watu wanaosherehekea siku hiyo hufanya mizaha na ujinga ili kupambana na nguvu ya kifo.
Neno Halloween lilianza tangu mwaka 1745 na lina asili ya Ukristo. Maana yake ni “Jioni Tukufu” (Holy Evening).

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini