Janga Jingine Lamkuta Emmanuel Mbasha, inadaiwa Kaficha Habari Kuhusu Mfanyakazi wake Aliyejinyonga ndani kwake.


Majanga yanazidi kumuandama aliyekua mme wa muimbaji maarufu Frola Mbasha, akiwa bado ana kesi mahakamani akidaiwa kumbaka ndugu yake hili ndio janga jingine lilimkuta Emmanuel Mbasha. Janga hilo ni la kufariki kwa mfanyakazi wake wa ndani ambae alijinyonga ijumaa iliyopita.

Inadaiwa kua Emmanuel na mfanyakazi huyo walikua wakiishi wawili tu ndani ya nyumba ya Emmanuel, lakini kitu cha kushangaza zaidi ni pale mfanyakazi huyo alipojinyonga. Inavyosemekana Emmanuel hakutoa taarifa kwa majirani kuhusu tukio hilo badala yake alitoa taarifa polisi na kisha kuusafirisha mwili wa marehemu kwa siri sana kwenda kumzika Singida.

Tumepata ujumbe kutoka kwa mmoja wa majirani wa Emmanuel Mbasha ambae hakutaka jina lake litajwe, ujumbe huo ulisema ” Kuna kijana wa kazi toka Singida alikuwa anaishi na Emmanuel Mbasha, amejinyonga na kuacha ujumbe kuwa kwa yaliyomkuta ameamua bora ajinyonge. Walikuwa wanaishi na Mbasha tu huko ndani na baada ya kujinyonga Mbasha amefanya siri kubwa mno hawakuweka hata msiba. Kijana alijinyonga Ijumaa na ndugu wakatafutwa wakaenda kureport polisi kwa ajili ya mazishi na wamemsafirisha kwenda kuzika Singinda. Mbasha hakuta majirani tujue. Mnaweza mtafuta kwa maelezo zaidi maana nikiandika hapa yeye ndo mwenye ukweli alimfanyia nini kijana wa watu.”

Bado tunafanya jitihada za kumtafuta Mbasha kwa ajili ya kuzungumzia suala hili…

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini