Balaa Sumbwanga: Wanachi Wachoma MOTO Vifaa Vya Kupigia Kura




Watu wapatao 200 wameteketeza  kwa moto vifaa vya kupiga kura  huku wengine wakiwajeruhi wasimamizi wa uchaguzi kwa kile kinachoonekana kuwa ni hofu ya kusambazwa kwa kura feki.


Katika tukio lililotokea wilaya ya Sumbawanga, watu hao wanadaiwa kuteketeza vifaa mbalimbali yakiwamo makasha  45 ya kuhifadhia   kura  wakidai kuwa yalikuwa na kura ambazo  tayari  zilikuwa  zimeshapigwa .

Akizungumza na mwandishi wa habari  hizi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda  amethibitisha kutokea  kwa tukio  huo  katika  kijiji  cha Zimba , Bonde la Ziwa Rukwa  wilayani Sumbawanga .

“Niko  njiani  nikielekea  katika eneo  la tukio  ni kweli  limetokea  usiku wa kuamkia leo  ….. vifaa hivyo  vilikuwa  vikisafirishwa  kwenda tarafa ya Milepa Bonde la Ziwa Rukwa  “ alisema

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Mwaruanda alidai kuwa watu wapatao 200 wakiwa na silaha za jadi yakiwemo  mapanga , marungu , mawe na  mikuki waliweka vizuizi  vya  mawe makubwa  barabara  kijijini Zimba  na kulizuia  gari  lililokuwa likisafirisha  vifaa  hivyo  vya kupiga kura  kwenda Tarafa ya Milepa.

Alieleza kuwa  gari hilo lenye  namba za usajiri T 865 BEU  likiwa na maofisa  wawili  wasaidizi wa uchaguzi  na dereva  lilizuiliwa na  watu hao  wenye hasira  na kuchoma  vifaa  vyote  vya  kupigia  kura  ambapo  watu wanane  wanashikiliwa na Jeshi la Polisi .

Kwa mujibu wa Mwaruanda  hakuna mtu yeyote  waliokuwa wakisafiri katika  gari hilo  aliyereruhiwa  katika tukio hilo ambao  majina yao  hayakuweza kufahamika mara moja  .

Kwa upande wake, Msimamizi wa Uchaguzi  wa Wilaya  ya Sumbawanga , Adam Missana  akizungumza na  mwandishi wa habari  hizi  kwa njia  ya simu  amekiri  kutokea kwa tukio hilo huo  akidai ulitokea  katika kijiji cha Zimba  kati ya saa tatu na nne  usiku wa kuamkia leo .

Missana ambaye pia ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Wilaya ya Sumbawanga  alidai kuwa  watu hao wenye hasira  wameteketeza   kwa kuchoma moto  vifaa vyote vya kupigia kura  zikiwemo karatasi  za kupigia kura  wagombea wa urais, ubunge , na udiwani .

“Vifaa  vilivyoteketezwa  kwa moto  ni pamoja na  masanduku ya kuhifadhia  kura  yapatayo 45 , taa , kalamu , karatasi  za wagombea urais , ubunge na madiwani “alisisitiza

Akifafanua aliongeza  kuwa  baada ya  kusambaza   vifaa vya  kupigia kura  katika Kata ya Zimba  walipofika  katika kituo  cha mwisho   ilikiwa tayari ni saa kumi na mbili  jioni  askari waliokuwa  wakisindikiza  gari  hilo  waligoma  kuendelea na safari kwa madai kuwa  wangefika Kata ya Milepa  usiku .

“Hata hivyo Msimamizi Msaidizi Jimbo, Charles Mwita  aliwaasa  askari polisi  waendeleee  na  msafari lakini walikataa  hivyo  gari  hilo  liliendelea na msafari  kuelekea Tarafa ya Milepa  bila  kuwa na ulinzi  wa askari polisi  hadi  walipo vamiwa na  watu hao  ambao  waliweka  vizuizi vya  mawe  barabarani  kijijini Zimba “ alisisitiza .

Aliongeza kueleza kuwa  gari hilo  lilipofika kijijini Zimba  watu wenye  hasira  walililizua  wakiwa na silaha mbalimbali za jadi “walishusha vifaa  vyote  vya  kupigia kura  kutoka garini  wakanyonya mafuta  kutoka kwenye  gari hilo  kisha wakayatumia  kuchomea  vifaaa hivyo “alisisitiza

“Maofisa Wasaidizi  wa Uchaguzi  wawili   na dereva wa gari  hilo  lililotekwa  wamejeruhiwa  na kuporwa  simu zao  na  vitu  vingine vya thamani “ alidai Missana .

Kwa mujibu wa Misaana  gari hilo  licha ya kuwa na maofisa wasaidizi wa uchaguzi  wawili  na wakitoka  kwenye mafunzo  ambao  baada ya gari hilo  kutekwa walifanikiwa kukimbia kusikojulikana .

Alieleza kuwa baada ya kuwasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  uchaguzi utakao fanyika leo katika Kata ya Milepa ni  wa Uraisi tu  kwa kuwa kwa taratibu za tume  uchaguzi wa Rais hauwezi  kuahirishwa .

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini