DIAMOND PLATNUMZ KAWEKA HISTORIA ULAYA

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Andrew Carlos na Musa Mateja
OKTOBA 25, mwaka huu ilikuwa ni moja kati ya siku za kihistoria nchini kwa Watanzania wote kujumuika na kupiga kura za kuwachagua wabunge, madiwani na rais.

Siku hiyohiyo pia katika Jiji la Milan, Italia kulikuwa na tukio la kihistoria kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye alikuwa akiiwakilisha Tanzania na Afrika kwa ujumla katika Tuzo za MTV Europe Music (EMA) na kufanikiwa kuibuka na ushindi kupitia kipengele cha Best Worldwide Act: Africa/India ambacho alikuwa akichuana na mwanamuziki maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi kuwa pia Miss World mwaka 2000.

Uso kwa uso na mastaa ulaya  
Kati ya matukio ambayo Diamond anasema hawezi kuyasahau ni pamoja na kupata shavu la kukutana na mastaa kibao wa ulaya ambao walipafomu na wengine kuchukuwa tuzo.

“Nimekutana na mastaa wengi ambao sikuwahi kukutana nao kabisa zaidi ya kuwaona tu kwenye mitandao na TV. Mastaa hao ni pamoja na Jason Deluro ambaye pia alipafomu Wimbo wa Want to Want, Pharrel Williams naye alipafomu Wimbo wa Freedom.“Nilipata bahati pia ya kuwashuhudia mastaa wengine kama vile Justin Bieber, Ed Sheeran na wengine kibao,” alisema Diamond.

Bieber anyakua 5 kwa mpigo
Staa wa Pop, Justin Bieber aliweka historia kwake katika tuzo hizo baada ya kuibuka na tuzo tano kwa mpigo.
Staa huyo aliyepanda jukwaani na kupiga ngoma yake mpya ya What Do You Mean alifanikiwa kuibuka na tuzo katika vipengele vya Best Male, Best Look, Worldwide Act: North America, Biggest Fans na Best Collaboration.
Mastaa wengine waliochukua tuzo hizo ni Nicki Minaj, One Direction, Macklemore, Taylor Swift, Ed Sheeran, Rihanna na wengine kibao.

Wazungu wapagawa na Diamond
Katika hali ya kushangaza mapema kabla ya kuanza kwa sherehe hizo za utoaji tuzo, Diamond aliyekuwa amevalia suti nyeupe alitinga ‘red carpet’ na kushangaa kuvamiwa na wazungu waliookuwa wamepanga foleni kuwasubiri mastaa huku kila mmoja akiwa na simu yake mkononi akitaka kupiga picha naye (selfie).

Washindi waliopita
Katika kipengele alichoshinda Diamond, alitanguliwa na Abdelfattah Grini (Morocco) aliyechukuwa mwaka 2011, Ahmed Soultan (Morocco) mwaka 2012 na 2013 na wa mwisho alikuwa Mohamed Assaf (Palestina).

Diamond anasemaje?
Kutokana na ushindi huo uliokuja Tanzania na Afrika kwa ujumla, Diamond alifunguka mengi ya kushukuru kwa wale wote waliompigia kura na kuahidi kufanya makubwa zaidi ya hayo katika kazi zake za muziki.

“Nimeshangazwa sana kwa namna ambayo nimepokelewa kwa kishindo nchini Italia. Wazungu wamenionesha thamani ya juu kwa mapokezi makubwa na kunishangilia na kunipongeza kwa tuzo niliyoipata. Nasema asanteni sana Watanzania wenzangu kwa sapoti mlionionesha mwanzo mwisho hadi kwa kunipigia kura na kufanikiwa kuibuka mshindi kutoka Afrika,” alisema Diamond.

Diamond alifanikiwa kupita tano bora Afrika katika Tuzo za Ema baada ya kupigiwa kura za kutosha na mashabiki wake kupitia mtandao wa Twitter. Wasanii wa Afrika aliokuwa akichuana nao kabla ya kutua Italia ni Yemi Alade (Nigeria), Davido (Nigeria), AKA (Afrika Kusini) pamoja na Wizkid (Nigeria).

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini