Breaking News: Tamko la LOWASSA Baada ya NEC Kumtangaza Dr MAGUFULI Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais Hivi Punde

Watanzania wenzangu!
Leo tarehe 29 October 2015, kwa kupitia
Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma
Duni Haji nimewasilisha rasmi
malalamiko yetu kuhusu mwenendo
mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi.
Tumeainisha kwenye malalamiko yetu,
kutokuridhishwa kwetu na mwenendo
na matukio mbalimbali, hususani,
utangazaji wa matokeo batili, yasiyo
akisi matokeo halisi yaliyopatikana
kwenye vituo vya kupiga kura, kama
ifuatavyo:
• Upunguzwaji wa kura zangu
• Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
•Tunaendelea kukataa dhuluma hii
dhidi ya matakwa ya wananchi, na
jaribio la kutaka kubakwa kwa
Demokrasia kunakooneka wazi
kutokana na mwenendo wa Tume
kuendelea kutangaza matokeo ya kura
yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi
wetu.
Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa
ushindi kwa wagombea wa vyama vya
UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na
Udiwani
Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu
sisi zilionesha kwamba nilikua
naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa
tumejiridhisha kwamba nimepata kura
10,268,795 sawa na asilimia 62% baada
ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu
za matokeo nchi nzima.
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa
ya Uchaguzi initangaze mara moja
mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa
mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri
Ya Muungano wa Tanzania.
Naendelea kuwashukuru wananchi kwa
imani yenu kwangu na kunichagua,
MImi, pamoja na viongozi wenzangu
tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia
ni kuvunja Amani, lakini sote
tunatambua ni nyie watanzania ndio
mnaoporwa haki yenu ya kupata
mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji,
hivyo nitaendelea kuwa pamoja na
watanzania wote kudai haki yenu kwa
nguvu zote.
Tanzania kwa miaka mingi
imefahamika kama kisiwa cha amani
katika Afrika, tunashangaa leo kuona
vyombo vya ulinzi na usalama
vikitanda kila mahali wakiwa na silaha
za kivita mitaani kana kwamba
uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha
wananchi ili wakubali kunyang’anywa
haki yao ya msingi ya kuchagua
viongozi wanao wataka, nina amini
watanzania hatutakubali hali hiyo.
Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini