Live Updates: MATOKEO RASMI Yote ya Ubunge Majimbo Mbalimbali Uchaguzi Mkuu 2015 Yanapatikana Hapa Kadri Yanavyotolewa


Tunawaletea matokeo rasmi kwa nafasi ya Ubunge kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yanavyotangazwa na Wakurugenzi wenye dhamana hiyo
Tembelea ukurasa huu mara kwa mara kwa updates zaidi

*********** 
Jimbo la Kilosa: Bawazir Mbaraka wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 55703, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Msabaha Mohamed wa Chadema, aliyepata kura 19632.
  
Jimbo la Babati Vijijini: Jitu Soni wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 56843, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Tara Surumbu wa Chadema, aliyepata kura 52683
Jimbo la Babati Mjini: Pauline Gekulu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 21970 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Chambiri Werema wa CCM, aliyepata kura 16434
   
Jimbo la Babati Mjini: Pauline Gekulu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 21970 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Chambiri Werema wa CCM, aliyepata kura 16434
Jimbo la Mbulu Vijijini: Flatei Massay wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 39911 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Aweda Petro wa Chadema, aliyepata kura 24109

Mkoani Rukwa katika Jimbo la Kalambo: Kandege Sinkamba wa CCM aibuka kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge kwa kupata kura 36,582 dhidi ya mpinzani wake Sichone Mateni wa CHADEMA kupata kura 31,102 

Jimbo la Tanga Mjini: Mussa Mbarouk wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 58675 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Omari Nundu wa CCM, aliyepata kura 57014

Jimbo la Arumeru Magharibi: Olemeiseyeki Gibson wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 94354 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Sabaya Thomas wa CCM, aliyepata kura 32831. 
Aliyekua mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd Azzan wa CCM
Mgombea Ubunge wa jimbo Kinondoni Maulid Mtulia aibuka mshindi katika jimbo hilo na kumshinda kwa kura aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kwa takribani miaka 10 Iddi Azzan.
Jimbo la Musoma vijijini: Prof. Sospeter Muhongo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41731 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Zakaria Mbura, aliyepata kura wa Chadema, aliyepata kura 24984
Jimbo la Iringa Mjini: Mchungaji Peter Msigwa pichani wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 43184 dhidi ya mpinzani wake wakaribu Fredrick Mwakalebela wa CCM, aliyepata kura 32406
Jimbo Kibamba: John Mnyika wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 79274 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Dkt.Fenella Mukangala wa CCM, aliyepata kura 55410
Jimbo la Morogoro Mjini: Abdulaziz Abood wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 99748, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Albanie Mathew wa Chadema, aliyepata kura 45502.
Qambalo Qulwi wa CHADEMA atangazwa kuwa Mbunge mtarajiwa toka Jimbo la Karatu, mkoa wa Arusha kwa kupata jumla ya kura 58,061 na kumtupa mpinzani wake Lorri Slaa wa CCM aliyepata jumla ya kura 32,444. 
Mary Nagu
Jimbo la Hanang: Mary Nagu wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 51997 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Derick Magoma wa Chadema, aliyepata kura 43841
Harrison George Mwakyembe ameibuka Mshindi wa ubunge katika Jimbo la Kyela kupitia tiketi ya CCM kwa kupata kura 44,269 dhidi ya mpinzani wake Hebel Abraham kwa kura 39,379
Aliyekua mbunge wa jimbo hili Dr. Cyril Chami
Jimbo la Moshi Vijijini, Kilimanjaro; Mgombea wa CHADEMA Anthony Calist Komu ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa jumla ya kura 55,813, akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Dr. Cyril Chami ambaye pia alishawahi kuwa Waziri Viwanda na Biashara aliyepata kura 24,415.
Heche John Wegesa
Jimbo la Tarime vijijini, mkoani Mara: Mgombea wa CHADEMA, Heche John Wegesa ameibuka kidedea kwa kupata kura 47,249, huku akifuatiwa kwa karibu na Kangoye Christopher Ryoba wa CCM aliyepata kura 42325. 
Mgombea wa CCM katika jimbo la Ilala, jijini Dar es salaam, Azzan Mussa Zungu ameibuka kidedea kwa kupata kura 35,818 dhidi ya kura 32,533 za Muslim Haiderali Hassanali wa CHADEMA.
Ezekiel Wenje
Jimbo la Nyamagana, Mwanza: Mgombea wa CCM, Mabula Stanslaus Shing'oma ameshinda kwa kuzoa kura 81,017, akifuatiwa kwa karibu na Ezekiel Wenje wa CHADEMA aliyeambulia kura 79,280. 
Bi. Angelina Mabula
Mgombea ubunge jimbo la ILEMELA jijini Mwanza Bi. Angelina Mabula (CCM) ameibuka mshindi kwa kupata kura 85,424 dhidi ya Highness Kiwia wa CHADEMA aliyepata kura 61679
mbatia
James Mbatia.
Jimbo la Vunjo: Mgombea wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa kura 60,187 akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Innocent Melleck Shirima aliyeambulia kura 16,097.
makamba
January Makamba.
Jimbo la Bumbuli: January Makamba (CCM) ameshinda kiti cha ubunge katika Jimbo la Bumbuli na kufanikiwa kutetea kiti chake.
Jimbo la Kawe: Halima Mdee (Chadema) ametangazwa rasmi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kawe akimwangusha mpinzani wake wa CCM, Kippi Warioba.
Jimbo la Mikumi: Mwanamuziki wa Hip hop, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia Chadema akipata kura 32259 dhidi ya Jonas Nkya (CCM) aliyepata kura 30425.
Jimbo la Temeke: Mgombea Ubunge (CUF) kwa Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo akipata kura 103,231 akimwangusha mpinzani wake Abbas Mtemvu (CCM) aliyepata kura 97,555.
Nape Nnauye
Nape Nnauye.
Jimbo la Mtama: Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama kupitia CCM, Nape Nnauye ameibuka mshindi katika jimbo hilo. Nape ameshinda kwa jumla ya kura 28110, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa CHADEMA, aliyepata kura 13918.
Jimbo la Ubungo: Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Saed Kubenea ameshinda ubunge wa jimbo hilo akimwangusha mpinzani wake Dk. Didas Masaburi wa CCM.
Jimbo la Kigamboni: Mgombea ubunge Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile (CCM) ameshinda ubunge wa jimbo hilo na kufanikiwa kutetea kiti chake.
Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa Chadema, aliyepata kura 13480.
Tundu-Lissu
Tundu Lissu.
Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM, aliyepata kura 18614.
Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema, aliyepata kura 16702.
Jimbo la Shinyanga Mjini: Bwana Steven Masele (CCM) ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini.
Jimbo la Serengeti: Marwa Ryoba (Chadema) ametangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kupitia tiketi ya Chadema katika jimbo la Serengeti. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe.
Jimbo la Chalinze: Ridhiwani Kikwete wa CCM, aibuka mshindi katika Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani kwa jumla ya kura 52695, dhidi ya Mang’unda Torongei wa Chadema aliyepata kura 23470.
Jimbo la Peramiho: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peremiho kwa tiketi ya CCM , Jenister Mhagama.
Jimbo la Mkinga: Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mkinga Dustan Kitandula ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Jimbo la Monduli: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, Ndugu Julius Kalanga ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Jimbo Buyungu: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza (CCM) 22,934. Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041. Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934. Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo.
Jimbo la Ismani: Wiliiam Lukuvi ametangazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ismani, mkoani Iringa kwa kuwa na jumla ya kura 26,119 na mpinzani wake Patrick Sosopi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa kwa kupata jumla ya kura 15,534
Jimbo la Ndanda: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215
MATHAYO
Dkt. David Mathayo.
Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa Chadema, aliyepata kura 15347
Jimbo la Same Mashariki: Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa kupata kura 18836, dhidi ya kura 15539 za Anne.
Jimbo la Mbogwe: Augustino Manyanda wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 32921, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Maganga Nicodemas Henry wa Chadema, aliyepata kura 13975
Jimbo la Mtwara Mjini: Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshindwa kukitetea kiti chake
Jimbo la Hai: Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura 51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya apata jumla ya kura 26,966.
Jimbo la Ngara: Alex Gashaza wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 53387, dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Dkt.Peter Bujari wa Chadema aliyepata kura 35254
Zitto Kabwe-ACT Leader3
Zitto Kabwe.
Jimbo la Kigoma Mjini: Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 31546, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Amani Kaburou wa CCM, aliyepata kura 16344
Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 54660, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa Chadema aliyepata kura 12580
Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi, aliyepata kura 14578
Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas Kalinde, aliyepata kura 18649
Jimbo la Njombe Kaskazini: Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini.
Jimbo la Dodoma Mjini: Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Dodoma Mjini.
Jimbo la Bukombe: Dotto Biteko (CCM) ameshinda ubunge Jimbo la Bukombe.
Jimbo la Kondoa Mjini: Edwin Sanda (CCM) ametangazwa mshindi Jimbo la Kondoa Mjini.
Jimbo la Chato: Dk Medad Kalemani Jimbo la Chato (CCM) ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 78817 dhidi ya mpinzani wake Benedicto Lukanima (Chadema) akipata kura 32513.
Jimbo la Bukoba Mjini: Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia Chadema, Wilfred Lwakatale ameibuka mshindi katika jimbo hilo kwa kumshinda mpinzani wake Khamis Kagasheki.
sugu
Joseph Mbilinyi (Sugu).
Jimbo la Mbeya Mjini: Mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi (Sugu) ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyengo Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894
Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura 14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata kura 13665
Jimbo la Sumbawanga Mjini: Aeshi Hilaly wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41763, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Ikuwo Malila wa Chadema, aliyepata kura 36183.
Jimbo la Lupembe: Joram Hongoli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe kwa kupata jumla ya kura 20,430 na kumwangusha mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Edwin Swalle aliyepata jumla ya kura 10407
Jimbo la Kasulu Mjini: Mgombea ubunge jimbo la Kasulu Mjini kupitia chama cha CCM, Daniel Sanze ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana huku akimbwaga mpinzani wake Moses Machali wa ACT Wazalendo aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo. Moses Machali amepata kura 22,512 wakati Daniel wa CCM amepata kura 25,336.
Jimbo la Kahama Mjini: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba (CCM), ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana.
Jimbo la Monduli: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli (CHADEMA), Julius Kalenga ametangazwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
bashe
Hussein Bashe.
Jimbo la Nzega Mjini: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Jimbo la Moshi Mjini: Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini, Japhary Raphael Michael (CHADEMA) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo kwa kupata jumla ya kura 51656 na kumuangusha Davis Mosha wa CCM.
Jimbo la Bunda Mjini: Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya (CHADEMA) ametangazwa rasmi mshindi wa jimbo hilo na kumuangusha Steven Wasira.
Jimbo la Siha: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584. Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).
Arumeru Mashariki: Joshua Nassari wa Chadema ameshinda ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki akipata kura 86694.
ESTER MATIKU
Ester Matiku.
Tarime Mjini: Ester Matiku wa Chadema ameshinda ubunge Jimbo la Tarime Mjini akipata kura 20,017,
Michael Kembati CCM akipata kura 14,025 na Deogratius wa ACT kura 336.
Lindi Mjini: Hassan Suleiman Kaunje (CCM) ametangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Manispaa ya Lindi, kuwa
Mbunge Mteule wa Jimbo la Lindi Mjini.
Mbinga Vijijini: Mgombea Martin Msuha (CCM) ametangazwa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi, Venance
Mwamengo kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Mbinga Vijijini baada ya kupata kura 59,269.
MAPUNDASixtus Mapunda.
Mbinga Mjini: Mgombea Sixtus Mapunda (CCM), ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Mbinga Mjini akipata kura 28,324.
Tunduma: Mgombea Mwakajoka Frank (Chadema) ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la
Tunduma (Mbeya) akipata kura 32,442. Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Halima Mpita.
Tandahimba: Mgombea Ubunge wa CUF katika Jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Ahmed Katani ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Musoma Mjini:  Mgombea Vedatus Mathayo (CCM) ametangazwa rasmi na Msimamizi wa Uchaguzi kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Musoma Mjini baada ya kupata kura 32,836.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini