Breaking News: Dr MAGUFULI Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Wa Kiti cha Urais wa Tanzania! MATOKEO Yote Jumla Haya Hapa

Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara
(NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji
Damian Lubuva imemtangaza Rasmi
mgombea Urais wa CCM, Dr John Pombe
Magufuli kuwa mshindi halali wa kiti
cha Urais katika uchaguzi mkuu
uliofanyika siku ya Jumapili wiki
iliyopita.
Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr Magufuli
amepata ushindi wa kura Milioni 8
( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.45%
huku akimwacha kwa mbali mpinzani
wake wa karibu , Edward Lowassa
(Chadema ) ambaye amepata jumla ya
kura Milioni 6 ( 6,077,848 ) sawa na
asilimia 39.97%
Dr Magufuli na mgombea mwenza,
Samia Suluhu watakabidhiwa rasmi
vyetu vya ushindi kesho saa nne
asubuhi katika ukumbi wa hoteli ya
Diamond Jubilee

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini