"Chonde chonde Rais Magufuli okoa Shule hii"


Serikali imeombwa kuiokoa Shule ya Msingi Ilembo katika kijiji cha Ilembo Mbeya Vijijini kutokana na shule hiyo kukabiliwa na uchakavu wa majengo, ukosefu wa madawati, nyumba za walimu na uchache wa Walimu.


Wakazi wa kijiji cha Ilembo wamesema hali hiyo imesababisha watoto wao kutopata elimu wanayostahili na hivyo kufanya vibaya kwenye mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.


Shule ya Msingi Ilembo, iliyopo katika kijiji cha Ilembo, Mbeya Vijijini, imejengwa mwaka 1954 na katika uhai wake wa miaka 61 imefanikiwa kutoa elimu kwa wakazi lukuki wa kijiji hicho ambao kwa sasa wanaendesha maisha sehemu mbalimbali mkoani Mbeya na mikoa mingine ya Tanzania.


Shule hii kwa sasa ipo dhoofulhali, ubovu wa madarasa, uchakavu wa madawati na uhaba wa walimu ni changamoto zinazoelezwa na wakazi wa Ilembo kuwa ni kikwazo katika utoaji wa elimu bora kwa watoto wao.


Malalamiko ya wananchi hao yanaungwa mkono na Mwenyekiti wa kijiji hocho, Anthony Ndege ambaye anasema kuwa serikali inapaswa kuharakisha ili kutatua changamoto hiyo kwani shule hiyo inategemewa na wananchi wengi wa kijiji hicho.


Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Juma Kenani, amesema angalau wameanza mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.


Changamoto hizo zinawasukuma baadhi ya wananchi waliosoma kwenye shule hiyo miaka kadhaa iliyopita kuitumia sikukuu ya Chrismas kutoa msaada wa madawati shuleni hapo kupitia Umoja wao unaojulikana kama Ilembo Family.


Shule ya Msingi Ilembo, ni miongoni mwa shule zilizopo maeneo ya vijijini ambazo zinahitaji juhudi za makusudi za wadau wa elimu na wananchi kwa ujumla ili kuziokoa na hali mbaya inazozikabili.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini