Mtumbwi wazama ziwani, watu wafariki wengine hawajulikani wako wapi


Watu watatu wamefariki baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kama kivuko cha kusafirisha abiria kutoka ufukweni kwenda kwenye boti ijulikanayo kama Mtu Ni Watu kuzama kwenye eneo la Mihama jijini Mwanza.


Ajali hiyo imetokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo, ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishna msaidizi mwandamizi Justus Kamugisha amethibisha kutokea kwa ajali hiyo


Takribani miaka ishirni tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba kilometa chache tu kabla ya kutia nanga jijini Mwanza bado mioyo ya watu ina simanzi kwa kuondokewa na wapendwa wao.


Yapo maelezo yasiyo na shaka kuwa baada ya baadhi ya abiria kuzuiwa kupanda meli mjini Bukoba walitafuta usafiri wa barabara hadi Kemondo ambapo waliingia kwenye meli na ilipopinduka na kuzama watu wengi walipoteza maisha.
Hayo yamejitokeza tena jijini Mwanza Mwaloni Kirumba ambapo wafanyakazi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA mbali na kuwazuia abiria waliotaka kusafiri na Boti ijulikananyo kama Mtu Ni Watu toka jijini Mwanza kuelekea kisiwa cha Goziba wilaya ya Muleba mkoani Kagera bado abiria hao walikodi pikipiki hadi ufukwe wa Mihama kuisubiria boti hiyo bila ya kujali zuio la SUMATRA.


Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Justus Kamugisha amesema tukio hilo ni matokeo ya kukaidi amri halali iliyowataka wamiliki wa boti hiyo ya mizigo kutoitumia kusafirisha abiria.
Kwa mujibu wa maelezo ya manusura wa ajali hiyo wamesema kuwa mtumbwi huo ulikuwa na abiria kumi idadi iliyokuwa inatolewa ufukweni kwenda kwenye boti kubwa.
Waliofariki katika ajali hiyo ni Rhobi Marwa mkazi wa Bunchali Tarime mkoani Mara, Rehema Magoke aliyekuwa muuzaji wa Duka la dawa kisiwani Goziba na Ismail Mazege mkazi wa Mihama jijini mwanza aliyekuwa nahodha wa mtumbwi uliozama.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini