Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari


1. UWATU

Uwatu

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa uwatu unao uwezo mkubwa katika kutibu kisukari. Uwatu huzisisimua seli katika kongosho kitendo kinachofanya uzalishwaji wa insulini kuongezeka. Maajabu haya ya uwatu yanasemekana kufanyika kutokana na uwatu kuwa na asidi amino mhimu sana ijulikanayo kama ‘4-hydroxyisoleucine’. Miaka mingi kabla hata ya huu utafiti kufanyika, uwatu umekuwa ukitumika kama moja ya dawa bora kabisa za asili katika kutibu kisukari.

Namna ya kuutumia Uwatu kujitibu kisukari

• Chota mbegu za uwatu vijiko 4 na uziloweke katika maji robo lita kwa usiku mmoja. Asubuhi ponda ponda hizo mbegu za uwatu ndani ya maji kisha zichuje na upate maji yake. Kunywa maji haya kila siku asubuhi kwa muda wa miezi 2.
• Chukuwa uwatu ya unga vijiko vikubwa 2 na uweke ndani ya maziwa au maji ya uvugu uvugu robo lita, koroga vizuri na unywe kila siku kutwa mara 2 kwa miezi 2.
• Chukuwa gramu 100 za mbegu za uwatu na gramu 50 za binzari manjano. Unaweza kuongeza kiasi kidogo cha pilipili manga nyeupe kwenye mchanganyiko huu. Ongeza kijiko 1 cha mchanganyiko huu wote katika maziwa robo lita na unywe kutwa mara 2 kila siku.
• Unaweza pia kuongeza uwatu ya unga katika unga wako unaotumia kutengenezea mkate au hata chapati.


2. MDALASINI

Mdalasini

Utafiti uliofanywa kwa watu wenye kisukari aina ya pili umeonyesha kuwa utumiaji wa gramu 1 hadi 6 za mdalasini kwa siku unaweza siyo tu kupunguza kaisi cha damu sukari mwilini, bali pia unaweza kupunguza kiasi cha mafuta mazito katika damu (triglyceride) na hata kudhibiti kolesto!

Waathirika wa kisukari pia hutokewa kuwa na matatizo katika mfumo wao wa upumuwaji, hivyo utumiaji wa mdalasini kwao unaleta maana zaidi kwakuwa mdalasini unao uwezo mkubwa katika kuzuia magonjwa katika mfumo wa upumuwaji pia. Mdalasini ya unga hushusha kiwango cha damu sukari kwa kuziamsha shughuli za insulini. Mdalasini pia ina faida kwa watu waliogunduliwa kuwa na kisukari cha mwanzo (pre-diabetes status) na hivyo matumizi ya mdalasini kwao yatasaidia kuzuia wasipatwe na kisukari katika siku za usoni.

Hata hivyo aina ya mdalasini unaotumia pia inahusika katika kutibu kisukari au maradhi mengine. Nashindwa kupata maneno haya kwa Kiswahili lakini kuna aina kama mbili hivi za mdalasini ambazo ni ‘Cassia cinnamon’ambao wenyewe huwa na kitu kingine ndani yake kiitwacho ‘coumarin’ ambayo ni sumu na husababisha matatizo katika ini. Mdalasini nzuri kwa kutibu kisukari na ambayo bei yake ipo juu kidogo ni ile iitwayo kwakiingereza kama ‘Ceylon cinnamon’.


Namna ya kutumia mdalasini kutibu kisukari

• Chukuwa lita 1 ya maji na uyachemshe. Mara yatakapoanza kuchemka, ongeza vijiko 3 vikubwa vya mdalasini ya unga na uache kwa dakika kama 15 hivi kisha ipuwa chuja na unywe ikiwa bado ya uvugu uvugu kutwa mara moja kila siku kwa mwezi 1.
• Ongeza mdalasini kijiko kidogo kimoja cha chai katika kikombe kimoja (robo lita) cha maji ya uvugu uvugu, koroga na unywe kila siku.
• Unaweza pia kuongeza mdalasini ya unga ndani ya kachumbari kila unapokula.


3. MAJANI YA MANJANO

Majano ya Manjano

Utafiti unaonyesha kuwa, kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini kama vile madini ya chuma, Zinki, na shaba; majani ya manjano ni mhimu sana katika kuutunza usawa wa glukozi katika damu. Madini haya huziamsha seli za kongosho zinazohusika na uzarishwaji wa homoni ya insulini. Majani ya manjano pia husaidia umeng’enywaji wa wanga mwilini. Yanao uwezo wa kuviamsha upya vimeng’enya katika figo na ini ambazo zinahusika katika kumeng’enya wanga na kuurudisha katika hali yake ya kawaida na hivyo kusaidia kutibu kisukari.

Wagonjwa wa kisukari huwa wana tatizo la kuwa na uwezo mdogo kudhibiti sumu mwilini jambo ambalo hupelekea seli zao za mwili kufa katika kiwango kingi. Utafiti unaonyesha kuwa majani ya manjano yana uwezo wa kupunguza kiasi cha seli kufa, seli ambazo ni mhimu katika uzarishwaji wa insulini.

Majani ya manjano yanaweza kushusha usawa wa damu sukari na ni mhimu sana kwa watu wanaopata kisukari kama matokeo ya uzito kuzidi. Ikiwa kisukari kinazunguka katika familia yenu, jitahidini kutumia majani ya manjano kwakuwa yamethibitika kuthibiti pia hata kile kisukari cha kurithi.

Namna ya kutumia majani ya manjano kujitibu kisukari

• Tafuna majani freshi ya manjano 7 mpaka 10 kila siku asubuhi.
• Tumia majani ya manjano kwenye kila chakula unachopika kila siku.

4. MSHUBIRI (Aloe Vera)

Mshubiri/Aloe Vera

Wakati mshubiri umekuwa ukitumika kwa miaka mingi katika kutibu kisukari, baadhi ya tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kuwa mshubiri unao uwezo pia katika kushusha kiwango cha damu sukari na mafuta katika mzunguko wa damu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na kisukari. Mshubiri umethibitika katika kutibu kisukari cha aina ya kwanza na hata cha aina ya pili.

Jinsi ya kuandaa mshubiri kutibu kisukari

Changanya vifuatavyo:
• Jeli ya mshubiri kijiko cha chai 1
• Unga wa majani ya matunda ya damu ya mzee kijiko cha chai 1
• Unga wa manjano kijiko cha chai 1

Kunywa mchanganyiko huu kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.

5. MAJANI YA MUEMBE

Majani ya Muembe

Wakati tunda la embe halina uwezo wa kutibu kisukari, majani ya mti wa muembe yanao uwezo huo! Waganga wengi wa Nigeria wamekuwa wakitumia sana majani ya muembe katika kutibu kisukari. Yanao uwezo wa kupunguza ufyonzwaji wa glukozi katika utumbo mkubwa hivyo kusaidia kupunguza usawa wa sukari katika damu. Pia yana uwezo mkubwa katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika damu.

Namna ya kuandaa


• Loweka majani 10 mpaka 15 ndani ya nusu lita ya maji kwa usiku mmoja. Chuja maji haya asubuhi mapema na uyanywe kabla ya kula chochote. Subiri lisaa limoja lipite ndipo ule chakula cha asubuhi.
• Kausha majani ya muembe kwenye kivuli. Yatakapokuwa yamekauka kabisa, yasage kupata unga wake na hifadhi unga huu katika chombo kisafi na kisha lamba unga huu nusu kijiko kidogo cha chai kila siku kabla ya chakula cha mchana na jioni.



6. MREHANI

Mrehani/Basil

Mrehani (basil) una faida nyingi sana kiafya. Nje ya kudhibiti kisukari, Mrehani pia una sifa na uwezo katika kudhibiti asthma, kuondoamfadhaiko, kudhibiti bakteria, kudhibiti virusi, kudhibiti vivimbe, kuondoa sumu mwilini, kudhibiti asidi tumboni, na kuongeza kinga ya mwili. Mrehani huzisaidia pia seli za kongosho kufanya kazi zake vizuri na kusaidia utolewaji au uzarishwaji mzuri wa insulini.

Jinsi ya kuutumia mrehani kutibu kisukari

• Tafuna majani mawili mpaka manne ya mrehani kila siku asubuhi kabla hujala chochote.
• Ponda majani ya mrehani kupata juisi yake kama kijiko kimoja hivi cha chai na unywe kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote.



7. BAMIA

Bamia

Bamia zina kiasi kingi cha vitamini A, B6, C, K, magnesium, potassium, zinki, na faiba. Bamia ina uwezo mkubwa katika kusawazisha usawa wa sukari mwilini. Mbegu za Bamia zina kidhibiti kiitwacho alpha-glucosidaseambacho huzuia wanga kujibadili kuwa glukozi. Faiba iliyomo kwenye bamia husaidia kurekebisha kiwango ambacho sukari humeng’enywa katika utumbo mkubwa.

Jinsi ya kutumia Bamia katika kujitibu Kisukari

Mahitaji:
• Bamia 2 mpaka 3
• Maji glasi 1

Jinsi ya kuandaa:
• Zisafishe bamia vizuri kabisa.
• Ondoa au ikate sehemu ya kichwa na mkia katika bamia na utupe. Kisha kata kila bamia katikati kwa urefu ili kupata vipande 2, hivyo utapata jumla vipande 4 kwa bamia hizo 2.
• Hivyo vipande 4 viweke ndani ya glasi iliyojaa maji, funika na uache hivyo kwa usiku mmoja.

• Asubuhi na mapema kunywa hayo maji yote yaliyokuwa na bamia kabla ya kula kitu kingine chochote. Ukiweza unaweza kula hata hizo bamia pia. Bamia mbichi zinafaida zaidi mwilini kuliko zilizopikwa.
• Fanya hivi kila siku kwa miezi kadhaa.

8. MBEGU ZA KATANI

Mbegu za Katani

Mbegu za katani zina kiasi kingi cha mafuta mhimu sana yajulikanayo kama “essential omega-3 fat alpha-linolenic acid (ALA)’’, pia zina protini, faiba na muunganiko wa mmea uitwao ‘lignans’. Hii lignans hufanya kazi kama kiuaji sumu au kwa maneno mengine hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini. Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mbegu za katani zinao uwezo wa kusawazisha usawa wa damu sukari mwilini kwa vile zina kiwango kikubwa cha faiba ndani yake. Mbegu za katani zinasaidia katika kazi za kumeng’enya chakula, pia husaidia katika ufyonzaji mzuri wa mafuta na sukari. Kama unatumia mara kwa mara hizi mbegu za katani, kiasi chako cha sukari chaweza kushuka hadi asilimia 28 kwa wakati mfupi.

Jinsi ya kutumia mbegu za katani katika kutibu kisukari

• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha unga wa mbegu za katani ndani ya glasi ya maji au maziwa na unywe wakati wa chakula chako cha asubuhi.
• Ongeza kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za katani katika nafaka zako unazotumia wakati wa chakula cha asubuhi.
• Ongeza pia unga wa mbegu za katani katika supu.

9. Chai ya Majani ya Mpapai

Majani ya Mpapai

Majani ya mpapai ni mazuri katika kuongeza ufanisi wa insulini. Ni mazuri kwa watu wenye kisukari cha aina ya pili. Pia majani ya mpapai husaidia kupunguza matatizo yawezayo kuwatokea watu wenye kisukari, matatizo kama vile mafuta kwenye ini, matatizo katika kibofu cha mkojo na pia husaidia kupunguza mfadhaiko/stress. Kuna faida nyingine kubwa zaidi ya kutumia majani ya mpapai ambayo ni uwezo wake katika kutibu vidonda vitokanavyo na kisukari kwa haraka zaidi. Waganga wengi wa tiba asili kutoka Japani na Australia Na wengine wengi toka mataifa mbalimbali wamekuwa wakitumia majani ya mpapai kutibu kisukari kwa miaka mingi sasa.

Mahitaji:
• Majani 10 ya mpapai
• Maji lita 2

Maandalizi:
• Tumbukiza hayo majani ya mpapai katika maji.
• Chemsha hayo majani katika maji kwenye moto hadi maji yatakapobaki nusu yake (lita 1).
• Ipuwa na uache ipowe
• Kunywa maji haya kidogo kidogo kutwa nzima. Fanya hivi kwa mwezi mmoja mpaka miwili.
Juisi hii ya majani ya mpapai iliyoandaliwa kwa mtindo huu ni nzuri katika kuondoa sumu mwilini na kurekebisha afya yako kwa ujumla huku ikirekebisha matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kuongeza kinga ya mwili wako.


10. Juisi mchanganyiko ya asili

Juisi ya Asili

Hii ni juisi nzuri sana kwa mtu yeyote anayesumbuliwa na kisukari na hatashinikizo la damu, vitu vingi vinavyoingia katika juisi hii ni tiba nzuri kwa magonjwa mengi mwilini. Hii ni juisi inayotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa vitu tofauti vifuatavyo.
Vitunguu swaumu 12
Vitunguu maji 12
Tangawizi 12
Asali ya nyuki wadogo lita 1
Ndimu 12
Chumvi ya mawe kijiko kidogo kimoja

Namna inavyoandaliwa

Saga (blendi) kwa pamoja vitunguu saumu na vitunguu maji pamoja na maji lita 2 na uchemshe kwenye moto kwa dakika kumi. Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake.

Saga tangawizi pamoja na maji lita 1 Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake, weka pembeni kwenye bakuli safi

Chukuwa limau au ndimu kata katikati kila moja na uchemshe kwenye moto na maji lita moja kwa dakika 15. zikishachemka subiri zipowe kisha zikamuwe na uchuje kupata juisi yake.

Changanya hizo juisi zote hapo juu katika chombo kimoja kikubwa na kisha

Ongeza asali ya nyuki wadogo mbichi nzuri lita moja, na mwisho ongeza chumvi ya mawe kijiko kidogo cha chai kimoja, koroga vizuri kwa pamoja.

Ukifuata vizuri maelezo haya mwishoni utapata juisi ya ujazo wa lita 5 au 6.

Kunywa juisi hii kikombe kimoja (robo lita) kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Juisi hii inaweza kukaa bila kuwekwa kwenye friji wiki 2 hadi 3 bila kuharibika.

VITU MHIMU VYA KUZINGATIA KWA MTU YEYOTE ANAYESUMBULIWA NA UGONJWA WA KISUKARI:
Acha kabisa soda ya aina yeyote pamoja na juisi za viwandani
Acha chai ya rangi na kahawa
Jishughulishe zaidi na mazoezi
Ongeza unywaji maji na utumiaji wa chumvi hasa ya mawe ile ya baharini
Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito ule unaotakiwa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
Tumia vyakula ambavyo havijakobolewa, mfano kama ni ugali tumiaunga wa dona na siyo wa sembe n.k

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!



Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini