Familia ya Leticia Nyerere kutoa kauli ya mwisho kuhusu afya yake


FAMILIA ya Leticia Nyerere, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) katika Bunge lililopita, itatoa tamko kuhusu hali ya afya ya mwanasiasa huyo Ijumaa wiki hii, baada ya kupata taarifa ya madaktari wanaomtibu.


John Shibuda ambaye ndiye msemaji wa familia, alisema jana kwamba kinachoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani amefariki dunia ni uzushi, kwa kuwa mgonjwa bado anaendelea kupata tiba kutoka kwa madaktari wake.

“Ninachoweza kukwambia ni kwamba kama familia tutatoa tamko rasmi Ijumaa kuhusu afya ya dada yetu na tutazungumza baada ya kupata taarifa za kina ya madaktari wanaomtibu,” alisema Shibuda.


Shibuda alisema kwa sasa hawana cha kuzungumza bali wanachojua ni kwamba ndugu yao bado anapata matibabu huko Marekani; 


“Tumeongea na madaktari watatupa taarifa zaidi Ijumaa na sisi hapo ndipo tutakapotoa taarifa kwa umma.”

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini