Mgonjwa Aliyetoa siri ya Muhimbili kwa Rais Magufuli alazwa chini

Yule mgonjwa aliyeibua ubovu wa mtambo ya CT Scan na mashine ya MRI kwa Rais John Pombe Magufuli, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar, Chacha Makenge (pichani)amekutwa na Uwazi akiwa amelala sakafuni wodini.


Desemba 25, mwaka huu, gazeti la Uwazi ambalo ni chanzo cha habari hii lilifika hospitalini hapo Jengo la Sewa Haji wodi namba 18 na kumshuhudia Chacha amelalia mashuka aliyoyatandika chini huku akiwa ameshusha neti tofauti na wagonjwa wenzake waliolala vitandani.


Chacha alisema, Desemba 24, mwaka huu, madaktari walimtaka ahame kwenye kitanda hicho kwa sababu kuna mgonjwa mwingine alipaswa kulazwa hapo.


“Mimi kitanda changu kilikuwa namba moja, sasa siku hiyo niliambiwa nimpishe mgonjwa mwingine aje kitandani kwangu ndiyo nikampisha na kuamua kulala chini kwa sababu walidai vitanda ni vichache wodini,” alisema Chacha.


Uwazi lilimtafuta afisa habari wa hospitali hiyo, Aminiel Eligaisha ili kumuuliza kuhusu kisa cha Chacha kulala chini wakati serikali hivi karibuni ilinunua vitanda 300 na magodoro yake kwa thamani ya shilingi Mil. 251 kwa ajili ya Taasisi ya Moi, lakini alisema yupo likizo na kutoa namba za msaidizi wake, Neema Mwangomo.
Neema yeye alisema suala la Chacha kulala chini au kinyume chake linahusiana na uongozi wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi). Alipopigiwa msemaji wa Moi, Almasi Jumaa simu yake haikupatikana hewani.


Novemba 9, mwaka huu, Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Moi ambapo alipata maelezo kutoka kwa uongozi sambamba na baadhi ya wagonjwa kumweleza kero yao.


Miongoni mwa wagonjwa hao ni Chacha ambaye alimwambia rais kuhusu ubovu wa mashine za CT-Scan na MRI akisema kuharibika kwake ndiko kunamfanya yeye aendelee kulazwa hapo kusubiri zipone na kufanyiwa vipimo. Rais aliagiza mashine hizo zitengenezwa haraka sana


Chanzo:Uwazi

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini