Mwaka unapoisha wafuatiliaji mbalimbali wa muziki huwa kwenye nafasi nzuri ya kuwafanyia tathmini wasanii kutokana na kazi walizofanya mwaka mzima, ambazo hutoa miongozo ya kutabiri nafasi ambazo wasanii hao wanaweza kuwa nazo katika mwaka unaofata. Mtangazaji wa BBC Radio 1 Xtra ya Uingereza, DJ EDu ametaja orodha ya wasanii wake watano wa kuwatazama zaidi mwaka 2016, kutokana na kufanya vizuri mwaka 2015. Katika orodha hiyo amemtaja muimbaji wa Tanzania, Vanessa “Vee Money” Mdee ambaye amemuweka kwernye nafasi ya 2. Wengine aliowataja ni 5. A pass (Uganda), 4. Runtown (Nigeria) 3. Donald (Afrika kusini) na 1. Ston bwoy (Ghana). Take note @djedu ’s Top 5 ones to watch in 2016 @IAmPass , @iRuntown , @DonaldInDenial , @VanessMdee + No.1 @Stonebwoyb pic.twitter.com/YCIj5TFBdL — BBC Radio 1Xtra (@1Xtra) January 3, 2016 Dj EDu huendesha kipindi cha chati ya muziki, DNA Top 5 ambayo hujuimuisha kazi za wasanii mbalimbali wa Afrika ikiwemo Tanzania. ASANTE KWA KUTEMBE...