Martin Kadinda aeleza Tanzania ina nafasi gani katika fashion kimataifa

Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda amesema Tanzania imepiga hatua nzuri katika mitindo kimataifa kutokana na bidhaa nyingi za wabanifu wa Tanzania kuchangamkiwa nje ya nchi. Kadinda ambaye alishinda tuzo ‘East African Fashion Designer of the Year’ nchini Kenya, ameiambia Bongo5 kuwaukiona Mtanzania anachukua tuzo kubwa nje ya nchi hiyo ni dalili kuwa wanafanya vizuri.
 “Kitendo cha Martin Kadinda kuwa best designer wa East Africa ni tumefika sehemu nzuri kwa sababu katika East Africa kuna nchi nyingi Kenya, Uganda, Rwanda Burundi. Kwahiyo itatuweka Tanzania sehemu nzuri ambayo hata makampuni makubwa wakihitaji kufanya kazi na wabunifu wataanza kuangalia Tanzania ndani ya East Africa,” alisema Martin.
Pia Martin amesema ndani ya mwaka 2016 atatoa suti tu na siyo kitu kingine kama alivyofanya 2015. 
“Namrudisha yule Martin wa miaka miwili iliyopita, Martin wa suti. Ukiongelea suti Tanzania utakuwa unamwongelea Martin kwa sababu hapo katikati nilikuwa nimeachia watu wengine kwa sababu hii ni biashara ya kupokezana uking’ang’ania kila kitu wewe siku ukiondoka pengo linakuwa kubwa ndio maana mimi mwaka uliopita nimebuni vitu vingi,” aliongeza.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini