Ditto ataja sababu za wasanii wapya kupotea
kama wasanii wangeamini wanachofanya pamoja na kuwa wabunifu, wangefanikiwa.
“Kitu kikubwa wanashindwa kuwa tofauti na wengine,” alisema.
“Mimi naona vijana wengi wapo hivyo, hawana ubunifu yaani kama ni waoga waoga hawaamini wanachokifanya
ndio maana wanaiga kile wanachokiona. Mimi nawashauri wajitahidi kuonyesha utofauti,
wafanye kazi kwa bidii hakuna kitu cha ajabu wote wamepitia huko huko,” alisema.