JKCI: Bado tunachunguza afya ya Pengo
“Bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi. Ikifika siku ya kumpa ruhusa ya kwenda nyumbani
kwake tutampa. Ila kwa sasa tunaendelea kumpa matibabu ili hali yake iimarike zaidi,” alisema
Profesa Janabi.
Alhamisi wiki iliyopita, Kardinali Pengo anayekaribia kufikisha miaka 72, alilazwa hospitalini
hapo baada ya hali yake kudaiwa kuwa mbaya.
Januari Mosi,
mwaka huu Rais John Magufuli akiwa ameambatana na mkewe Janeth
walimtembelea kiongozi huyo wa kiroho na kufuatiwa na viongozi wengine wa kitaifa na wa dini.
waliokwenda kumwona Kardinali Pengo juzi ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo aliyekwenda jana.
Mwingine ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa ambaye aliwataka
waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania wazidi kumwombea Kardinali Pengo.
Katibu wa Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Aidan Mubezi alinukuliwa juzi akisema
Kardinali Pengo akitoka hospitalini atazungumza vyombo vya habari juu ya afya yake.
Oktoba15, mwaka 2014 wakati akihutubia kwenye ibada maalumu ya misa iliyoandaliwa na
Utume wa Wanaume Katoliki (Uwaka),
Jimbo la Dar es Salaam Pengo alizungumzia afya yake
baada ya kutoonekana hadharani kwa muda mrefu kutokana na kuumwa.
Hata hivyo, katika ibada hiyo hakutaja ugonjwa unaomsumbua.