Wema Sepetu: Sitafuti kiki kupitia nyimbo za Diamond (Video)

Wema Sepetu ameachana na Diamond Platnumz na kujikuta wakiwa kama paka na panya lakini inaonekana kuwa mrembo huyo ameshindwa kujizuia kuacha kuufurahia muziki wa staa huyo wa Nana.

Wiki chache zilizopita, video inayomuonesha Wema akiwa na Aunty Ezekiel wakiimba wimbo wa Diamond, Utanipenda ilisambaa mtandaoni baada ya kuipost kwenye Snapchat. 
Na sasa Wema amerejea tena na wimbo mwingine wa ex wake huyo, Mdogo Mdogo. Awamu hii wimbo huo unasikika ukipigwa kwenye redio ya salon aliyokuwa akirembwa lakini alionesha kuufurahia na kushare clip kwenye snapchat. Hata hivyo muigizaji huyo anaonya kuwa hatafuti kiki kupitia nyimbo za ex wake kama wengine wanavyoweza kufikiria. “Haiya hii sasa nadhani kwa wale wenye akili finyu mtaanza ooooh nyimbo,” ameandika kwenye Instagram. “Jamani eeh Radio hio ilikuwa inafanya kazi yake and I was busy with snapchat….!!! Maana walimwengu wa sasa bila kujishuku lazima mseme…. Khaaaa…!!!! Msije mkasema natafuta kiki bure na wakati Kiki nilizonazo zanitosha mieeeeee….. I dont need more…. Add me on snapchat @wemasepetu or Tz Sweetheart…. Dada dee nini eeh….?”

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini