Wananchi Kupanga Nauli za Mabasi Yaendayo Kasi
MAMLAKA ya Udhibiti,Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), inatarajia kukusanya maoni ya wananchi juu ya viwango vya nauli za mabasi yatakayotoa huduma ya usafiri wa haraka Jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa SUMATRA kwa vyombo vya habari kwenda kwa wananchi ambapo ofisi hiyo itawaalika wadau wote wa usafiri hususani wananchi kuchangia maoni kwenye mkutano utakao fanyika januari 5 kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 na nusu asubuhi.
Mamlaka pia inapokea maoni ya wananchi kupitia anuani ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo ambayo ni S.L.P 3093 au kwa barua pepe ambayo info@sumatra.go.tz ambapo kabla ya kufikia uamuzi wadau wanatakiwa kutoa maoni ya kuridhia viwango vya nauli kwa mujibu wa sheria ya Sumatra.
Maoni ya maandisi yatapokelewa kwenye ofisi ya Mkuregenzi Mkuu iliyopo Jengo la Mawasiliano House Makutano ya barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Nkumo kuanzia Saa 4 asubuhi hadi saa 9 alasiri mwisho wa kupokelewa maoni hayo ni Januari 13 mwaka huu.
Mamlaka hiyo imepokea maombi ya nauli kutoka kampuni ya UDA-RT inayolenga kutoa huduma ya mpito ya usafirishaji jijini Dar es Salaam katika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa Dart.
Maombi yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ni Safari kwenye njia za pembeni (feeder route) shilingi 700 ,safari kwenye njia kuu (trunk route) shilingi 1200 na njia zote mbili ni 1400 ambapo wanafunzi watalipa nusu nauli anayotoa mtu mzima.