Skip to main content

Halotel kufikisha mtandao kwa asilimia 95 ya watanzania hadi mwishoni mwa mwaka 2016


Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo kuhusuiana na mtandao huo kutanua huduama zake hadi kufikia asimimia 95 ya watazanzania. Wanaoshuhudia ni Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Emanuel Malyeta (kushoto), na kulia kwake ni mwanasheria wa kampuni hiyo,Christopher Masai.


Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Halotel, Emanuel Malyeta akifafanunua jambo kwa waandishi wa habari. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai kulia kwake ni mwanasheria wa kampuni hiyo, Christopher Masai.


Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akimkabidhi zawadi mwandishi wa gazeti la the Guardian, Sylivester Domaso.

Kampuni mpya ya simu za mikononi, Halotel, leo imetangaza mpango wake wa kufikisha mtandao wa simu kwa asilimia 95 ya watanzania hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Wakiongozwa na kauli mbiu yao yaPamoja katika Ubora, wanalenga kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na simu ya mkononi pamoja na kupata huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo havikuwa vimeunganishwa na huduma ya mtandao awali.

Hadi sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano, kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95% ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.

Akizungumzia mipango ya kampuni yake kwa mwaka 2016, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Halotel, bwana Le Van Dai amesema kampuni yake itaendelea kupeleka mtandao katika vijiji vingine 1500 katika mwaka 2016 na kuweka mkazo wa hali ya juu katika mrejesho kwa wateja pamoja na kuboresha mtandao, huduma kwa wateja, huduma kwa jamii hali itakayopelekea mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini.

‘Kampuni yetu itashirikiana na watanzania katika kuhakikisha inaleta maendeleo kwa watanzania, kama ambavyo kauli mbiu yetu ilivyo, Pamoja katika Ubora, ndivyo ambavyo tutaendelea kuwekeza hapa nchini hali itakayopelekea kukua haraka kwa kampuni yetu’ alisema Bwana Dai.

Katika hatua nyingine Dai amewashukuru watanzania na serikali yao kwa mapokezi waliyoipa kampuni yao, na pia amewahakikishia kuwa Halotel itaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na wataendelea kushirikiana nao katika kusukuma maendeleo ya nchi.

‘Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa waliotupa, na kuelekea mwaka 2016, kampuni yetu itaendelea kukuza ubunifu, zawadi pamoja na huduma nyingine kwa wateja wetu’ alisema Dai.

Kwa mwaka 2015 pekee, kampuni ya Halotel imelipa kodi ya zaidi ya dola milioni 27 za kimarekani, ambayo kati ya hiyo dola milioni 24 imetumika kulipa kodi uingizaji bidhaa na dola laki saba ni kodi inayohusuiana na rasrimali watu.

Dai amesema pia kampuni yake imetengeneza zaidi ya ajira 1,500 za moja kwa moja na zaidi ya 20,000 za ajira zisizo za moja kwa moja, akisisitiza kuwa kampuni yake itahakikisha inafata sheria za ajira za Tanzania.
Katika hatua nyingine, Dai alielezea masikitiko yake kwa matukio ya wizi na uporaji wa mitambo ya Halotel, akielezea kuwa zaidi ya matukio 52 yameripotiwa kuanzia mwezi wa kwanza hadi Disemba mwaka huu, ambapo imewasababishia hasara ya jumla ya shilingi milioni 393.
Lengo la Halotel ni kuhakikisha kila mtanzania ana simu ya mkononi ili kubadilisha namna watanzania wanaishi na namna wanavyokuza na kujenga uchumi wao.
‘Kampuni yetu ina zaidi ya kilomita 18,000 za fibre optic, pamoja na zaidi ya minara 2500, hivyo kuifanya Halotel kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini, ambayo pia itatumika kuunganisha serikali za mitaa 150, hospitali 150, vituo vya polisi 150, ofisi za posta 65 na intaneti ya bure kwa shule zaidi ya 450’ alimaliza Dai.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …