Mbunge Professor JAY Kutimiza Ahidi Hii Jimboni Kwake Mapema

Ni headlines za mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule aka Professor Jay ambaye amezungumza na ripota wa millardayo.com kuhusiana na kutekeleza kile alichokiahidi wakati wa kampeni.

‘Ni kweli na moja kati ya vitu nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu ni kwangu niliwambia wananchi kwamba wakinipa ubunge katika jimbo la Mikumi basi nitahakikisha kuwa naboresha sekta mbalimbali ikiwemo sanaa, ambapo wasanii waishio Mikumi watakuwa wakirekodi kupitia studio ya Mwanalizombe’ – Professor Jay 


‘Studio yangu ya Mwanalizombe nitaileta Mikumi kuanza kazi muda si mrefu kuanzia sasa tumeshaleta baadhi ya vifaa hapa kwahiyo Mwanalizombe Studio iliyokuwa Dar es Salaam kuanzia sasa hivi itakuwa inapatikana Mikumi jimbo kwangu’ – Professor jay

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini