Lukuvi: Tunataka nyumba nafuu za ukweli
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
kuandaa mpango wa haraka wa mradi wa kujenga nyumba za
gharama nafuu utakaokuwa na ukweli wa unafuu huo
Alitoa agizo hilo jana alipotembelea ofisi za shirika hilo mkoani
hapa.
Alisema kuanzia sasa, NHC lazima ibuni mbinu rahisi za
kujenga nyumba bora ambazo zitauzwa kwa gharama nafuu ya
ukweli kuliko zinazouzwa sasa ambazo alisema wananchi wengi
wanashindwa kuzinunua kwa sababu bei yake ni kubwa.
‘‘Acheni kuilalamikia Serikali kwa kuchukua fedha za Ongezeko la Thamani (VAT) kwenu kwamba
ndiyo inayoongeza gharama za ujenzi, fanyeni utafiti wa namna ya kuanza kujenga nyumba bora
na za gharama nafuu kiukwelikweli ambazo mnaweza kujenga mijini na hata kwenye miji midogo midogo vijijini’’ alisema.
Lukuvi alisema Watanzania wamechoka kusikia taasisi zinatangaza kwamba zinajenga nyumba za
kuuza kwa gharama ndogo wakati bei inakuwa kubwa sawa na nyumba za kuuza kibiashara.
Awali,
Meneja wa NHC Mkoa wa Mbeya unaojumuisha na Mkoa wa Njombe, Juma Kyaramba
alimweleza waziri Lukuvi kwamba wanaendelea na ujenzi wa nyumba za kuuza wilayani Mbarali
na Makete ambazo zitauzwa kwa bei nafuu.
Kyaramba alisema NHC Mbeya ambayo ina majengo 42 yenye maeneo zaidi ya 200 ya
kupangisha, ilikusanya zaidi ya Sh1 bilioni mwaka jana na mwaka huu inatarajia kukusanya 1.3
bilionii.
Pia, waziri Lukuvi alikagua madeni ya wateja ambayo yanafikia Sh43 milioni kubwa likiwa la
Sh30.5 milioni la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Sh9.9 deni la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Sh3 milioni inazoidai Hospitali ya Rufaa Mbeya