Wasanii mwaka 2016 uwe wa kazi na si lawama – Fella
Fella ambaye ametambulisha kundi jipya la muziki liitwalo Salam TMK, alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV
kuwa mwaka 2016 utakuwa mwaka mwema kama wasanii watautumia vizuri.
“Ninaweza nikawaambia wasanii wajibrand vizuri, lawama ndogo ndogo hazihitajiki tena mwaka 2016,” alisema.
“Kama kuna lawama zinahitajika basi ni za jumla au ziwe lawama kama mtu kaonewa au amenyanyaswa lakini
tusilalamike ilimradi kugomea vitu wakati tunajua serikali yetu imeamua mpaka kutuwekea waziri ambaye
atatusikiliza na kusikiliza matatizo yetu kwa maslahi yetu. Kwahiyo tunatakiwa kuwa wamoja na tutengeneze unity
nzuri ili tufikie malengo yetu kwa pamoja,” aliongeza.