Matatu kutoka Ikulu kwa Rais Magufuli leo January 4…




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wanne Ikulu, Dar es salaam.

Taarifa kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa alisema Rais Magufuli alikuwa na na mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad kuhusu kupunguza gharama za matumizi ya kuendesha serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Prof. Mussa Juma Assad akizungumza na Rais Magufuli.

Prof. Assad ameagizwa pia na Rais Magufuli kuhakikisha Tanzania inaongeza ukusanyaji wa mapato kutoka 14% ya pato la Taifa.

Rais Magufuli pia amekutana na Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania, (DPP) Biswalo Eutropius Mganga ambaye amesema mazungumzo yao yalihusiana na mikakati ya namna ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inavyopaswa kufanya kazi ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo “Hapa Kazi Tu”.

Rais Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mashtaka Bw. Biswalo Eutropius Mganga

Kiongozi Mwingine aliyekutana na Rais Magufuli ni Mufti Mkuu wa Tanzania SheikhAbubakar Zuber Ally ambaye amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri.

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber Ally akizungumza na Rais leo Ikulu


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini