Waziri Mwigulu NCHEMBA Atumbua Majipu Mengine!

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba jana alifanya ziara ya siku moja kukagua mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa ya ranchi ya Taifa ya Ruvu. 

Akiongea na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo, Waziri Nchemba alisema ujenzi wa ranchi hii ya Taifa ya Ruvu ulianza mwaka 2010 lakini hadi sasa haujakamilika kutokana na uzembe na kukosa uzalendo kwa baadhi ya watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia mali hii ya Umma. 
Kutokana na uzembe huo, waziri Nchemba amefanya maamuzi yafuatayo;



==>Kwanza,amewasimamisha wakurugenzi wote wa bodi ya (NARCO) kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa kwa kushindwa ama kwa maksudi au vinginevyo kusimamia ujenzi wa machinjio haya ya kisasa.

Alisema Bodi hii imesababisha Taifa lipoteze Billion 5.7 zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa hatua za awali za machinjio haya. 
==>Pili,amesitisha kuendelea kwa kazi kwa mkurugenzi wa ranchi za Taifa kwa kushindwa kusimamia mradi huu ulioliingizia Taifa hasara ya Bilion 5.7 

==>Tatu,ameagiza ndani ya siku 7 kupitia wataalam wa wizara wahakikishe wanampelekea ripoti ya thamani ya fedha inayohitajika kumalizia ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa 

==>Nne,ameagiza wahusika wote walioshiriki kuliingizia Taifa hasara hii wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria kwaajili ya hatua za kinidhamu. 


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini