Matapeli 15 wa viwanja wadakwa
Zaidi ya watu 15 wamekamatwa kwa tuhuma
za uvamizi na uuzaji wa viwanja vya watu katika Mtaa wa
Kulangwa, Kata ya Goba Manispaa ya Kinondoni katika kipindi
cha wiki moja.
Kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Wazo kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli wa uuzaji wa
viwanja vya watu vikiwamo vilivyotengwa na manispaa kwa
shughuli za kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kulangwa,
Shafii
Mkwepu alisema vitendo hivyo vimekithiri katika mtaa huo.
Mkwepu alidai kuwa matapeli hao ambao wanamtandao mkubwa, wamekuwa wakiuza viwanja mbalimbali vya wananchi kwa kutumia mihuri feki ya ofisi ya serikali ya mtaa huo.
“Matapeli hawa hutangaza kuwa kuna viwanja vinauzwa na Manispaa, hivyo watu wengi
wamekuwa wakitoka maeneo mbalimbali na kuja katika mtaa wa Kulangwa kwa ajili ya kupimiwa
viwanja hivyo, hapo ndipo huwalizwa na matapeli hao,”
alidai Mkwepu na kuongeza:
“Kutokana na tatizo hilo, wananchi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama,
tumefanikiwa kuwakamata watu 15 ambao wanasadikiwa kuhusika na utapeli huu.”
Alisema inadaiwa watu hao wamejipatia fedha zaidi ya Sh80 milioni baada ya kuuza viwanja
hivyo.
Alisema hiyo ni mara ya pili kwa watu hao kufanya utapeli huo.
“Tunalaani kitendo hiki na ninawahakikishia wananchi kuwa viwanja vyao vitakuwa salama na mpaka sasa Manispaa haijatoa taarifa kuhusu uuzaji wa viwanja hivyo ila wananchi nao
wanatakiwa kuwa makini na matapeli hao,” alisema.
Alisema wiki iliyopita matapeli hao walivamia kiwanja cha shule ya Oktavian Tema chenye
ukubwa wa heka nne walichotaka kukiuza, bahati nzuri hawakufanikiwa baada ya Serikali ya Mtaa
kupata taarifa na kuweka ulinzi.
Hata hivyo, itakubukwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alishawahi kusema
kuwa wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya migog