Je, Mnatambua Kuwa Baadhi ya Maamuzi ya MAGUFULI, Yanaligharimu Taifa Kiuchumi?

Kuna watu wanashangilia sana kila kinachofanywa na Magufuli, wakidhani ndio the right thing!. Mfano alipoamua kuunda baraza dogo la mawaziri, na kuongeza idadi ya makatibu wakuu, badala ya kupunguza gharama, kutaongeza ghara za uendeshaji!, serikali ni makaribu wakuu ambao ndio waendeshaji, na sio mawaziri!.

Mfano wanaposikia maofisa wakuu fulani wa umma, wamesimamishwa kazi, na kuteuliwa wengine kukaimu nafasi zao!. Hatua hii kisiasa ni nzuri, maana ina mpa kick Magufuli kwa boost political mileage yake, ila kiuchumi, Magufuli analibebesha taifa hili mzigo kubwa kuliko hata serikali ya JK!.

Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila mtumishi aliyesimamishwa kazi kwa tuhuma zozote, anaendelea kulipwa mshahara wake kamili, bali maupurupu ndio yanaondolewa!.

Mtumishi atalipwa nusu ya mshahara iwapo atasimamishwa kazi na kushitakiwa, na mtumishi hatalipwa lipwa mshahara iwapo atafukuzwa kazi!


Tangu Magufuli aanze hii timua tumua, hakuna ofisa mkuu yoyote aliyefukuzwa, wala aliyeshitakiwa, wate wamesimamishwa tuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!, wote wanaendelea kulipwa mishahara yao ile ile!.

Hata upande wa uteuzi wa Makatibu Wakuu, wale makatibu wakuu wote ambao ukatibu wao mkuu haukutenguliwa, wanaendelea kulipwa mishahara ya makatibu wakuu kusubiri kupangiwa kazi nyingine!.

Hivyo baadhi ya hatua zinazochukuliwa na rrais wetu John Pombe Magufuli, japo ni hatua nzuri, na zimefanywa kwa nia njema, zitaligharimu sana taifa hili!, ni bora Magufuli angefuata ule mtindo wa Nyerere, ilikuwa hakuna kusimamisha kazi, ilikuwa ni kufukuza tuu!. Anapounda baraza jipya na kutea makatibu wakuu wapya, wale wote walioachwa, walikuwa wanastaafishwa kwa manifaa ya umma na mishahara yao inasimamishwa kuanzia hapo!.
Happy New Year
By Pasco-JF

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini