IRENTE VIEW POINT LUSHOTO TANGA, MOJA YA KIVUTIO AMBACHO WATU WENGI HAWAJAKITAMBUA.
Hapa ndipo kileleni na Mwonekano wa Irente
Hii ni Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo hili kwa upande kwa Kushoto.
Eneo hili wakazi wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia picha
Hii ni njia ya kuelekea Pangoni
Ukiwa Juu ndani ya Pango utaona hivi
Mmoja wa wandishi wa Blogs za Mikoa Fredy Tony akiwa amefika kujionea eneo hilo.
Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda kufanya utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa jiji.
Irente View Point inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani lushoto mkoani Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na wengine walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada hasa wakati wa sikukuu za Christmas
Eneo hili lina urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza kuona maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.
Jinsi ya kufikia ikiwa unatokea upande wowote, fika hadi Mombo, panda daladala Tsh 3,000 mpaka Lushoto mjini baada ya hapo unaweza panda Boda boda Tsh 3,000 au ukachukua Tax Tsh 10,000 , kiingilio ni Tsh 2,000.