Picha Za Basi Lililotumbukia Mtoni na Kuua+Kujeruhi

WATU watatu wamekufa baada ya basi la abiria lenye namba za usajili T 922 BUW aina ya Yutong mali ya kampuni ya AL- Hushoom, kutumbukia kwenye mto Lukosi eneo la Msosa, Iyovi, Wilayani Kilosa, mkoa wa Morogoro baada ya kugonga kingo za daraja na kuparamia miti miwili
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema leo kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nane mchana, wakati basi hilo likitokea jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya.
Miongoni mwa waliokufa ni dereva wa basi hilo. Wapo majeruhi 16, kati yao 14 walilazwa katika Kituo cha Afya cha Mtandika kilichopo eneo la wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa na wengine sita walisafirishwa hadi hospitaali ya mkoa wa Iringa na kulazwa huko.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini