Profesa Mwesiga BAREGU Amvaa MAGUFULI... Amkosoa Vikali Uteuzi wa Viongozi Alioufanya

Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amekosoa uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu alioufanywa hivi karibuni na rais John Magufuli. 

Profesa Baregu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema kuwa anaushangaa uteuzi huo kwani unakinzana na dhana yake ya kutaka kupunguza ukubwa wa serikali yake. 
“Tulitarajia kuwa rais Magufuli angechagua idadi ya makatibu wakuu ambayo inaakisi baraza lake la mawaziri, lakini nimeshangaa kuona kwamba kwenye baadhi ya wizara kuna makatibu wakuu wawili au watatu,” Profesa Baregu aliliambia The Citizen.


Aliongeza kuwa hivi sasa ni vigumu kufahamu kuwa nani atakuwa mtendaji mkuu kwenye wizara ambayo wameteuliwa makatibu wakuu wawili au watatu. 

Naye Mkurugenzi wa Sheria katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia aliungana na kauli ya Profesa Baregu na kueleza kuwa ni vyema sasa sheria ikaweka ukomo cha idadi ya watu wanaopaswa kuteuliwa kwenye ofisi husika.


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini