Kagame kugombea muhula wa tatu, Marekani yalaani
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa tatu wa Urais baada ya wananchi kupigia kura
rasimu ya katiba inayomruhusu kufanya hivyo.
Akihutubia taifa hilo siku ya mwaka mpya, Kagame alidai kuwa uamuzi wake huo umetokana na chaguo la
wananchi wake.
Wananchi wa Rwanda waliipigia kura rasimu ya katiba hiyo December 18 kumruhusu Kagame, 58, kuwania tena
muhula mwingine wa urais mwaka 2017 wenye miaka saba.
Katiba hiyo itamruhusu kuwania tena mihula mingine miwili ya miaka kumi hadi mwaka 2034.
Hata hivyo Marekani imelaani vikali hatua hiyo.