Posts

Showing posts from 2016

Watch & Download (Official Video) Pam D Ft Mesen Selekta - Popo lipopo

Image
                                                       WATCH HERE                                                      DOWLOAD HERE ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Watch & Download (Official Video) Danagog ft. Davido – Hookah

Image
WATCH VIDEO                                                    DOWLOAD VIDEO  ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Mtangazaji wa BBC Radio 1 Xtra ya Uingereza amtaja msanii wa Tanzania wa kutazamwa zaidi 2016

Image
Mwaka unapoisha wafuatiliaji mbalimbali wa muziki huwa kwenye nafasi nzuri ya kuwafanyia tathmini wasanii kutokana na kazi walizofanya mwaka mzima, ambazo hutoa miongozo ya kutabiri nafasi ambazo wasanii hao wanaweza kuwa nazo katika mwaka unaofata.  Mtangazaji wa BBC Radio 1 Xtra ya Uingereza, DJ EDu ametaja orodha ya wasanii wake watano wa kuwatazama zaidi mwaka 2016, kutokana na kufanya vizuri mwaka 2015. Katika orodha hiyo amemtaja muimbaji wa Tanzania, Vanessa “Vee Money” Mdee ambaye amemuweka kwernye nafasi ya 2. Wengine aliowataja ni 5. A pass (Uganda), 4. Runtown (Nigeria) 3. Donald (Afrika kusini) na 1. Ston bwoy (Ghana). Take note @djedu ’s Top 5 ones to watch in 2016 @IAmPass , @iRuntown , @DonaldInDenial , @VanessMdee + No.1 @Stonebwoyb pic.twitter.com/YCIj5TFBdL — BBC Radio 1Xtra (@1Xtra) January 3, 2016 Dj EDu huendesha kipindi cha chati ya muziki, DNA Top 5 ambayo hujuimuisha kazi za wasanii mbalimbali wa Afrika ikiwemo Tanzania. ASANTE KWA KUTEMBE...

Tyga matatani, ni kwa kudaiwa kumtongoza binti wa miaka 14 kwenye Instagram (Video)

Image
Hivi ndivyo msichana huyo alivyosema: “I’m very upset that a story about Tyga, Kylie Jenner and me was published in OK! Magazine and I want people to know the truth. The truth is that Tyga contacted me first. He direct­messaged me on Instagram. I knew who he was, but I was surprised that he was contacting me. I thought that it could possibly be about my music but he did not mention that in his initial communication. I thought that was strange but I was thinking he would bring it up in his next message to me. However, he didn’t mention in the next message.”  “I began to feel uncomfortable when he asked me to FaceTime with him. He asked me to FaceTime three times but I didn’t do it. Because of my discomfort with why he wanted to communicate with me, I quickly stopped responding. I never sent the communication between Tyga and me to OK! Magazine and I don’t know how they obtained them. I would never have allowed OK! Magazine or any other magazine to use them. It is also upsetting ...

Ditto ataja sababu za wasanii wapya kupotea

Image
Msanii na mtunzi wa nyimbo, Lameck Ditto amesema wasanii wengi wachanga wanashindwa kufanikiwa kutokana na woga pamoja na kutokuwa wabunifu kwa kukopi kazi za wasanii waliowakuta kwenye game. Ditto ambaye pia kwa sasa amejikita kwenye kilimo cha biashara, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa,  kama wasanii wangeamini wanachofanya pamoja na kuwa wabunifu, wangefanikiwa. “Kitu kikubwa wanashindwa kuwa tofauti na wengine,” alisema. “Mimi naona vijana wengi wapo hivyo, hawana ubunifu yaani kama ni waoga waoga hawaamini wanachokifanya ndio maana wanaiga kile wanachokiona. Mimi nawashauri wajitahidi kuonyesha utofauti,  wafanye kazi kwa bidii hakuna kitu cha ajabu wote wamepitia huko huko,” alisema. ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Professor J kuihamishia studio yake Mikumi

Image
Msanii mkongwe wa Hip Hop na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’, amesema ana mpango wa kuihamishia studio ya Mwanalizombe kwenye jimbo lake ili aweze kutekeleza ahadi ya kuinua sanaa.  Akizungumza na gazeti la Mtanzania Jumatatu hii, Professor Jay alisema moja ya ahadi alizowaahidi wakazi wa Mikumi kwenye kampeni zake ni kuibua vipaji vipya. “Mikumi kuna vipaji vingi vya muziki lakini hakuna aliyeweza kuviibua kwa miaka mingi, ila mimi nikiwa kama Mbunge wao nitatekeleza ahadi hii kwa kuihamishia studio yangu Mikumi ili wasanii chipukizi waweze kufanya kazi zao,” alisema Profesa Jay.  Mwanalizombe ni studio inayomilikiwa na msanii huyo ipo maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es salaam na imeshatoa nyimbo kali kama Makamanda wimbo wa Sugu, Tatu Chafu na Kipi Sijasikia chini ya mtayarishaji Villy.  ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Lukuvi: Tunataka nyumba nafuu za ukweli

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuandaa mpango wa haraka wa mradi wa kujenga nyumba za gharama nafuu utakaokuwa na ukweli wa unafuu huo Alitoa agizo hilo jana alipotembelea ofisi za shirika hilo mkoani hapa. Alisema kuanzia sasa, NHC lazima ibuni mbinu rahisi za kujenga nyumba bora ambazo zitauzwa kwa gharama nafuu ya ukweli kuliko zinazouzwa sasa ambazo alisema wananchi wengi wanashindwa kuzinunua kwa sababu bei yake ni kubwa.  ‘‘Acheni kuilalamikia Serikali kwa kuchukua fedha za Ongezeko la Thamani (VAT) kwenu kwamba ndiyo inayoongeza gharama za ujenzi, fanyeni utafiti wa namna ya kuanza kujenga nyumba bora na za gharama nafuu kiukwelikweli ambazo mnaweza kujenga mijini na hata kwenye miji midogo midogo vijijini’’ alisema.  Lukuvi alisema Watanzania wamechoka kusikia taasisi zinatangaza kwamba zinajenga nyumba za kuuza kwa gharama ndogo wakati bei inakuwa kubwa sawa na nyumba za kuuza kibiash...

Wagundua tiba ya Ukimwi

Image
Wakati dunia ikiwa na zaidi ya watu 34 milioni wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), madaktari nchini Hispania wametangaza kugundua tiba ya ugonjwa huo wanayodai ni uhakika. Kwa kutumia damu ya kupandikiza kutoka kwenye kitovu mwana (umbilical cord) cha mtu ambaye ana vinasaba ambavyo havipokei virusi hivyo vya Ukimwi,  wataalamu hao wa tiba wa Hispania wanaamini kuwa wanaweza kutibu ugonjwa huo baada ya mafanikio waliyopata kwa mgonjwa mmoja. Madaktari hao wa Kitengo cha Taifa cha Upandikizaji (ONT) cha Hispania walichukua damu ya vitovu mwana vya watu wenye vinasaba ambavyo havipokei VVU na kuipandikiza kwa mtu anayeishi na virusi hivyo. Baada ya miezi mitatu, mgonjwa huyo alipimwa na kuonekana hana virusi. Daktari wa Programu ya Upandikizaji kutoka Taasisi ya Tiba ya Catalan, Barcelona, Rafael Duarte alisema mgonjwa aliyetibiwa kwa njia hiyo,  Timothy Brown (37), alikuwa anaishi na VVU tangu mwaka 2009 na madaktari hao walithibitisha kuwa amepona baada ya kupandikiz...

Mambo shaghalabaghala Jangwani

Image
Wakati muda wa `mapumziko’ ya bomoabomoa ukimalizika leo huku jaribio la kupata zuio la muda likiwa limewekwa kiporo, wakazi wa Jangwani ambako nyumba zitaanza kubomolewa leo, jana waliweka mabango barabarani yanayotuma ujumbe wa aina mbalimbali kwa Rais John Magufuli. Bomoabomoa hiyo ilianza Desemba mwaka jana likilenga nyumba zilizojengwa kwenye Bonde la Mto Msimbazi, lakini lilisitishwa kwa siku 14 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5,  mwaka huu kuwapa nafasi wakazi kuondoka kwa hiari yao kuokoa mali zao. Wakazi wa Jangwani walitumia mwanya huo wa kusitisha ubomoaji, kufungua kesi Mahakama ya Ardhi kupinga kuondolewa maeneo hayo bila ya kupatiwa sehemu nyingine na kuwasilisha ombi za zuio la ubomoaji, lakini chombo hicho cha sheria kilikataa kubariki mambo hayo ya kutaka sitisho la bomoabomoa liendelee wakati kesi ikiendelea mahakamani.  Wakati wawakilishi wa wakazi hao wakiwa mahakamani katikati ya jiji, watumishi wa...

Mauaji ya ‘Tajiri Mtoto’ yaendelea kuzua utata

Image
Mtandao wa kikundi kinachozalisha pombe kali bandia kinachodaiwa kuwa na uhusiano na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), unahusishwa na mipango ya kumuua mfanyabiashara Joseph Mahole maarufu ‘Tajiri Mtoto’.  Mfanyabiashara huyo aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Desemba 30, mwaka jana nyumbani kwake eneo la Katanini, Wilaya ya Moshi Mjini. Mauaji hayo ambayo yameibua utata hasa baada ya wauaji hao kudaiwa kuondoka na bastola tu iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu na hawakuchukua kitu kingine chochote.  Habari kutoka kwa marafiki wa karibu na marehemu, zinadai huenda njama za kumuua zilifanywa na baadhi ya watumishi wa TRA na wafanyabiashara wanaozalisha pombe kali bandia. Kwani baada ya upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Mahole, Polisi waligundua kuwapo kwa malighafi ya kutengenezea pombe kali pamoja na vifungashio vyake. Pia, walizikuta stika zenye nembo ya TRA zinazobandikwa kwenye chupa za pombe kuonyesha kuwa bidhaa in...

Kura Yangu Nilimpa Rais MAGUFULI, Lakini Kwa Sasa Naijutia

Image
Binafsi wakati wa kampeni nilivutiwa sana na sera ya Rais Magufuli ya kuipunguza serekali yake kwa nia ya kubana matumizi.  Na nia yake hiyo njema kwa taifa masikini Kama Tanzania ndio ilinishawishi nikiri nikampa kura yangu ya ndio. Ila kwa sasa nimeanza kukata tamaa kwa uteuzi aliofanya Rais wa kuteu makatibu wengi watakao turudisha pale pale tulipokuwa tunalia lia kuwa serekali ni kubwa mno na isiyokuwa na mashiko.Inayoumiza wananchi wake.Ni kiri wazi nimeanza kuijutia KURA yangu na next time Ccm sitowaamini tena na siwaamini tena hata sasa hivi.  -By Kibo10 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Profesa Mwesiga BAREGU Amvaa MAGUFULI... Amkosoa Vikali Uteuzi wa Viongozi Alioufanya

Image
Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amekosoa uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu alioufanywa hivi karibuni na rais John Magufuli.  Profesa Baregu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema kuwa anaushangaa uteuzi huo kwani unakinzana na dhana yake ya kutaka kupunguza ukubwa wa serikali yake.  “Tulitarajia kuwa rais Magufuli angechagua idadi ya makatibu wakuu ambayo inaakisi baraza lake la mawaziri, lakini nimeshangaa kuona kwamba kwenye baadhi ya wizara kuna makatibu wakuu wawili au watatu,” Profesa Baregu aliliambia The Citizen. Aliongeza kuwa hivi sasa ni vigumu kufahamu kuwa nani atakuwa mtendaji mkuu kwenye wizara ambayo wameteuliwa makatibu wakuu wawili au watatu.  Naye Mkurugenzi wa Sheria katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia aliungana na kauli ya Profesa Baregu na kueleza kuwa ni vyema sasa sheria ikaweka ukomo cha idadi ya watu wanaopaswa kuteuliwa kwenye ...

LULU Michael Afunguka Kuhusu Kula Uroda na TEKNO, Aanika Kila Kitu!

Image
Elizabeth ‘Lulu’ Michael amelazimika kuandika maelezo marefu kukanusha tetesi zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa alivunja amri ya sita na hitmaker wa Duro, Tekno aliyekuwepo Dar siku ya mwaka mpya. Haya ni maelezo yake aliyoandika kwenye Instagram:Okay…naona watu Mnatafutaga Topic Na mkipata picha story mnatungaga mnazozijua NI hivi….naomba heshima Na busara vitumike Nilikutana Na Tekno Kwenye show yake Na alikuja kunisalimia kwenye meza Yangu,picha zote zilizopigwa Na yeye au mtu mwingine yoyote zilipigwa kwenye meza yangu by the time amekuja kunisalimia,Na sio mm tu niliyepiga nae picha NI watu wengi. Kuhusu issue yake Na whoever called Gigy me cjui Coz hata sikuwepo wakati wanapigana picha zao…Kwahyo mni exclude kwenye hyo issue Yao Nilikuwa najua akili Za watu wengi NDO maana hata sikuthubutu kupost picha yangu Na Tekno B4 this issue Mnachotakiwa kujua….nilienda kwenye show as a fan n nothing else [blush] Na NDO maana hata Post alopost Na mm ka post Kwa heshma N...

Waziri Mkuu Awaonya Wanyonyaji wa Wakulima... Aziagiza Halmashauri Kujenga Vituo vya Ununuzi Vijijini Badala ya Kuendelea Kutumia Mawakala

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea, wakati akiendelea na ziara yake mkoani Ruvuma.  Akizungumza na wafanyakazi wa Wakala hiyo, wadau wa kilimo pamoja na wananchi jana, (Jumatatu, Januari 4, 2016) nje ya majengo ya Wakala mara baada ya kukagua mahindi yaliyohifadhiwa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea , mkoani Ruvuma alisema kufuatia taarifa ya kuwepo na baadhi ya maeneo yenye njaa nchini, Serikali imetoa tamko kuwa hakuna mtanzania atayakekufa kwa njaa.  Alisema serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa imeweka mikakati ya kukabiliana na tatizo la njaa kwa kutoa msaada wa chakula katika maeneo yanayokabiliwa na njaa.  “Ni wajibu wangu kuhakikisha nasimamia vizuri hili, nimeona hali ya uhifadhi wa chakula, tunayo mahindi ya kutosha lakini hakuna sehemu ya kuhifadhi chakula” alisema Waziri Mkuu.  Waziri Mkuu Majaliwa ...

Profesa Mwesiga BAREGU Amvaa MAGUFULI... Amkosoa Vikali Uteuzi wa Viongozi Alioufanya

Image
Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amekosoa uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu alioufanywa hivi karibuni na rais John Magufuli.  Profesa Baregu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema kuwa anaushangaa uteuzi huo kwani unakinzana na dhana yake ya kutaka kupunguza ukubwa wa serikali yake.  “Tulitarajia kuwa rais Magufuli angechagua idadi ya makatibu wakuu ambayo inaakisi baraza lake la mawaziri, lakini nimeshangaa kuona kwamba kwenye baadhi ya wizara kuna makatibu wakuu wawili au watatu,” Profesa Baregu aliliambia The Citizen. Aliongeza kuwa hivi sasa ni vigumu kufahamu kuwa nani atakuwa mtendaji mkuu kwenye wizara ambayo wameteuliwa makatibu wakuu wawili au watatu.  Naye Mkurugenzi wa Sheria katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia aliungana na kauli ya Profesa Baregu na kueleza kuwa ni vyema sasa sheria ikaweka ukomo cha idadi ya watu wanaopaswa kuteuliwa kwenye ...

Mwanamuziki Maarufu Auawa Baada ya Kupambana na Polisi na Kupigwa Risasi

Image
Visa vya watu kuuawa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara Bujumbura  Mwanamziki mmoja kutoka Burundi amepatikana amefariki katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura baada ya kukamatwa na polisi, hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kundi la wanahabari la SOS.  Taarifa hizo zinasema kwamba mwili wa Pascal Tresor Nshimirimana ulipatikana Jumamosi eneo la Musaga, karibu na gereza kuu la Bujumbura.  Polisi wanasema Pascal alijaribu kumnyang'anya bunduki afisa wa polisi, na akauawa na risasi ililofyatuka kutoka kwa bunduki hiyo kwa bahati mbaya. Bw Nshimirimana alikuwa mmoja wa waandamanaji ambao walipinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza  Katika kisa kingine, mwili wa kiongozi wa vijana William Nimubona ulipatakana katika maeneo ya Kavuma jijini Bujumbura.  Hata hivyo, hakuna taarifa huru za kudhibitisha mauaji ya kiongozi huyo. Bw Nimubona alikuwa kiongozi wa mrengo wa vijana katika chama cha National Liberation Forces (N...

KUBENEA Linda Heshima yako katika Jamii... Sifurahishwa na Uhasama Uliopo na ZITTO KABWE

Image
Watanzania tumekuwa na mila na desturi ya kupongezana pale tunapofanya vizuri na pia kukosoana tunapofanya vibaya. Ni kutokana na utamaduni huu nathubutu kukuandikia. Awali ya yote mimi ni msomaji wa magazeti ya Mwanahalisi/Mawio ambayo wewe kama mmiliki au mwandishi wa habari unapitishia taarifa zako kwenda ktk jamii. Nimeguswa kukuandikia baada ya kusoma matoleo ya magazeti yako mawili ukionyesha kuwa na vita baridi na Zitto Zuberi Kabwe. Mimi kama msomaji ninayejinyima pesa yangu ili kununua gazeti lako hakika sifurahishwi saana kusoma uhasama uliopo kati yako na Zitto Kabwe. Tumetoka ktk uchaguzi na kama Taifa tunahitaji kutoka hapa tulipo kwenda mbele zaidi. Hatuwezi kufikia malengo kama uhasama uliopo kati yako na Zitto unataka kutuambukiza sisi wasomaji kupitia gazeti lako, na wala hatuwezi kwenda mbele tukiwa na hulka tuliyotoka nayo huko nyuma. Tambua nafasi uliyonayo ktk jamii kwa sasa ya Ubunge kwa maana ya mwakilishi wa wananchi hivyo unatakiwa tabia...

Watumishi wa kada za afya nchini watakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili na viapo vya taaluma zao

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa Geita.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA). Wauguzi wa wodi ya akinamama katika hospitali teule ya mkoa wa Geita. Tabibu wa kituo cha afya Nyankumbu, Abdallah Kiroboto akimsikiliza Waziri Ummy mara alipoingia kwenye chumba cha kutolea huduma, pembeni ni mama aliyefika kituoni hapo na watoto wake kupata matibabu. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwlimu akisalimiana na wagonjwa kwenye kituo cha afya Nyankumbu mkoani Geita alipotembelea kituo hicho. Wagonjwa waliofika hospitalini hapo wakisubiri huduma kwenye hospitali hiyo. Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu mara ba...

Breaking News: Kesi ya kupinga bomoabomoa Kinondoni yasogezwa mbele hadi saa 8 mchana

Image
Baadhi ya wananchi ambao wamekumbwa na wengine wakiwa bado hawajafikiwa na bomoabomoa hiyo wakiwa wamekaa nje ya mahakama kuu ya ardhi kusubiri hatma yao Kesi ya kupinga kubomoa nyumba katika mabonde ya Kinondoni ambayo ilikuwa isikilizwe jana jumatatu na kuhairishwa hadi leo jumanne, januari 5 imehairishwa kwa muda kusikilizwa hadi saa nane mchana. Tayari magari ya Polisi ya washawasha na vikosi vya ulinzi vimetanda nje ya mahakama kuu ya ardhi kwa ajili kuhakikisha kunakuwa na hali ya usalama katika eneo hilo. ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!! LIKE PAGE  YETU KWA  HABARI  ZAIDII

Jeshi la Polisi mkoani Singida lamshikilia mtu anayedhaniwa kuwa jambazi sugu

Image
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP.Thobias Sedoyeka. Na Nathaniel Limu, Singida Jeshi la polisi mkoani Singida,limefanikiwa kukamata mkulima na mkazi wa Kibaoni Iddy Issah (33), anayedhaniwa kuwa ni jambazi sugu baada ya kulipiga risasi moja mguu wake wa kulia, wakati alipojaribu kutoroka. Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP Simon Haule,alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa Januari tatu mwaka huu saa 7.20 usiku katika baa ya Leaders iliyopo kata ya Kindai tarafa ya Unyakumi manispaa ya Singida. Alisema siku ya tukio askari polisi walipokuwa kwenye doria katika mitaa ya kata ya Kindai, walipata taarifa za kiintelijensia kuwa mtuhumiwa yupo baa ya Leaders maeneo ya Kibaoni. “Baada ya polisi hao kupata taarifa hizo,walifika haraka kwenye baa hiyo na kujaribu kumkamata mtuhumiwa.Lakini alipambana nao huku akitaka kumnyang’anya silaha mmoja wa askari polisi hao,hata hivyo,hakuweza kufanikiwa”,alisema Haule. Kaimu kamanda huyo,alisema baada mt...

Halotel kufikisha mtandao kwa asilimia 95 ya watanzania hadi mwishoni mwa mwaka 2016

Image
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo kuhusuiana na mtandao huo kutanua huduama zake hadi kufikia asimimia 95 ya watazanzania. Wanaoshuhudia ni Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Emanuel Malyeta (kushoto), na kulia kwake ni mwanasheria wa kampuni hiyo,Christopher Masai. Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Halotel, Emanuel Malyeta akifafanunua jambo kwa waandishi wa habari. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai kulia kwake ni mwanasheria wa kampuni hiyo, Christopher Masai. Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akimkabidhi zawadi mwandishi wa gazeti la the Guardian, Sylivester Domaso. Kampuni mpya ya simu za mikononi, Halotel, leo imetangaza mpango wake wa kufikisha mtandao wa simu kwa asilimia 95 ya watanzania hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Wakiongozwa na kauli mbiu yao ...