BASATA Adhabu Hii Kwa SHILOLE ni Kubwa Mno!

Baraza la Sanaa la taifa, BASATA limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa shughuli za sanaa zinaenda katika mstari unaotakiwa.
BASATA limedai kumfungia Shilole kutojihusisha na muziki kwa mwaka mmoja kwa madai ya kuidhalilisha Tanzania kwa kusambaa picha za aibu alizopigwa wakati anatumbuiza nchini Ubelgiji miezi kadhaa iliyopita 
11330616_296972493806688_1211325526_n
Na kwa kiasi kikubwa baraza limekuwa likijitajidi kuipigania sanaa ya Tanzania kwa namna nyingi ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kuanzisha na kusimamia tuzo za muziki za Tanzania, Kilimanjaro Music Awards pamoja na mambo mengine.

Miongoni mwa masuala mengine ambayo BASATA imekuwa ikifanya ni kusimamia maadili kwenye sanaa na kutoa onyo ama adhabu kwa wanaoyakiuka.

Katika kipindi cha hivi karibuni, BASATA imetoa adhabu mbili kubwa ambazo ni pamoja na kuyafungia mashindano ya Miss Tanzania kwa miaka miwili na adhabu waliyoitoa jana ya kumfungia Shilole kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja.

BASATA imetoa adhabu hiyo baada ya miezi kadhaa iliyopita picha za aibu za Shilole kusambaa mtandaoni wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji. Kwa mujibu wa Shilole, picha hizo zilipigwa na mmoja wa watu waliokuwa wakiangalia show yake na kuzipost kwenye mitandao ya kijamii. Picha hizo zinaonesha maziwa ya msanii huyo wazi na kiukweli sio picha nzuri.

“Nasisitiza tena sikudhamiria na wala sikupenda hiyo kitu itokee, ila nasikitika kwamba kama mimi mwanamke yule mtu aliyenipiga picha na kudhamiria kuziweka kwenye mitandao alikuwa na maana gani, hakufikiria mimi nitaunmia kiasi gani au mashabiki wangu wataumia kiasi gani? Ni mtu mbaya mwenye roho mbaya sijui nimuiteje huyo mtu aliyefanya hivyo, sio mtu mzuri,” Shilole alisema kwenye mahojiano aliyofanya.

BASATA walitoa maelezo kueleza namna walivyosikitishwa na picha hizo na kumuita Shilole aendee kujieleza. Kwa mujibu wa Shilole, aliliomba radhi baraza hilo pamoja na mashabiki wake.

Shilole anaamini kuwa kama aliweza kuomba radhi zaidi ya mara moja, adhabu hiyo haikupaswa kutolewa.

Maoni yangu ni kuwa kitendo alichofanya Shilole kilipaswa kuadhibiwa lakini sio kwa ukubwa huu wa sasa. Adhabu ya kutojihusisha kwenye muziki kwa mwaka mmoja kwa muimbaji anayetegemea muziki na tena mwanamke mwenye familia ni kubwa mno.

BASATA walipaswa kufikiria kuwa adhabu hii haitoishia kumuumiza Shilole peke yake, bali hata familia yake. Shilole ana watoto wawili wa kike anaowasomesha kupitia muziki. Anasomesha pia watoto wawili wengine wa ndugu zake.

Na kwa familia zetu nyingi za Kitanzania, ni wazi kuwa ndugu wengi wa karibu wa Shilole humtegemea kwa namna moja ama nyingine. Wategemezi hawa watapata tabu kubwa kutokana na mama yao kukatiwa chanzo kikuu kinachomuingizia fedha – shows.

Adhabu hiyo inamaanisha kuwa Shilole atakaa mwaka mzima bila kufanya show yoyote, ndani wala nje ya nchi. Kwa mwaka mzima ataishi vipi?

Kwa haraka haraka, BASATA ikishikilia msimamo wake, Shilole itabidi atafute njia nyingi ya kujipatia kipato. Ni wazi kuwa huo utakuwa ni mwanzo wa kumtoa msichana aliyekuwa amejiajiri kwenye muziki kuingia kwenye shughuli zisizofaa kama vile kujiuza au kufanya biashara haramu. Madhara yake baada ya hapo ni makubwa zaidi.

Adhabu hii ikitimizwa, itamuathiri pia msichana huyu kisaikolojia na kiukweli athari haziwezi kuwa ndogo. Wote tunafahamu ukali wa maisha ulivyo miaka hii na kwa msichana kukatiwa vyanzo vyake vya kiuchumi kwa mwaka mzika ni adhabu kubwa mno.

Ninawasihi BASATA kuzingatia athari za adhabu hii kwa si tu Shilole, bali wanae na watu wengine wanaomtegemea. Nashauri waipunguze adhabu hii kwa kumlipisha pengine faini ambayo pia itakuwa fundisho si tu kwake bali kwa wasanii wengine.

Ujumbe umeshafika na tena kwa sauti kubwa kuwa BASATA halitaki kabisa mchezo, lina mamlaka na kwamba wasanii wanapaswa kuwa makini kwenye kazi zao kwa kuepuka kutumia vilevi wanapokuwa jukwaani.

Fundisho ni kuwa wasanii wachukulie muziki kama ajira zingine kwa kujistahi wao wenyewe na mashabiki wao. Watambue kuwa nidhamu ya kazi ni miongoni vitu muhimu vitakavyowasaidia kutunza heshima za majina yao.

Watambue kuwa matukio kama haya yatawakosesha fedha nyingi kutoka kwa makampuni ambayo hayapendi kujihusha na wasanii wenye sifa mbaya midomoni mwa watu.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini