KUMEKUCHA! LOWASSA AFUNGUKA MAZITO WAKATI AKITANGAZA KUHAMIA CHADEMA RASMI LEO

Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ametangaza rasmi kukihama chama cha mapinduzi, CCM mchana huu na kutangaza kuhamia CHADEMA.....

Lowassa ametoa kauli hii Bahari Beach , Dar akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa UKAWA ambao wamekutana na waandishi wa habari kuzungumzia hatima yake kuelekea ikulu pamoja na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.

Lowassa amesema baada ya kutafakari kwa kina na kujiridhisha, ameamua kujiondoa CCM kwa kuwa siyo baba yake wala mama yake na kuitikia wito wa UKAWA kupitia CHADEMA.

Amesema safari yake haitafanikiwa iwapo hatajitokeza watu wengi kupiga kura na anaiomba tume ya uchaguzi iongeze muda ili watu wote waweze kujiandikisha

Lowassa amesema alinyimwa haki yake na CCM kama mtanzania kujieleza na kujitetea, hivyo atakuwa mnafiki akisema ana imani na chama hicho
Baada ya maelezo hayo; Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe alisimama na kumkabidhi rasmi Lowassa Kadi ya CHADEMA.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini