LIVE! BATULI wa BongoMovies Anaswa CHUMBANI na Mwanaume Wakifanya Yao!

BATULI STAN BAKOLA (1) 
Muigizaji mwenye mvuto wa aina yake Bongo Movies, Yobnesh Yussuph ‘Batuli’  katika mahaba mazito na mchekeshaji Stan Bakora.
Musa mateja 
DAH! Wakati mashabiki wake wakiamini si mtu wa ‘kurukaruka’ kivile, muigizaji mwenye mvuto wa aina yake Bongo Movies, Yobnesh Yussuph ‘Batuli’ amekwaa aibu baada ya picha zake zikimuonesha akiwa kimahaba chumbani na mchekeshaji Stan Bakora kuvuja, Ijumaalinakupa mchapo kamili.
BATULI STAN BAKOLA (5)TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo kilichovujisha ubuyu huo kilieleza kuwa, kina picha zinazomuonesha Batuli akiwa kimahaba na Stan bila kujua walizipiga kwa ajili gani.
“Nina picha za Batuli akiwa na kanga moja, anaonekana yuko na Stan Bakora ‘on bed’, sijajua wamezipiga za nini ila ukiziona nadhani unaweza kuzifanyia kazi,” kilidai chanzo hicho.
BATULI STAN BAKOLA (6)Ijumaalazinasa
Baada ya picha hizo ambazo kimsingi ziko kinyume kabisa na maadili ya Kitanzania (kwenye filamu haziwezi kuonekana na hata kwenye gazeti haziwezi kuchapishwa) kutua kwenye dawati la gazeti hili, jitihada za kupata undani wake zilianza kwa kuwatafuta wahusika.
BATULI STAN BAKOLA (4)Bofya hapa kumsikia Batuli
Paparazi: Mambo Batuli?
Batuli: Safi vipi kuna usalama huko maana asubuhi sana hii?
BATULI STAN BAKOLA (7)Paparazi: Huku usalama upo isipokuwa kuna picha uko na Stan Bakora, vipi ndiyo umeamua kujiweka mazima?
Batuli: Mmmh… Tafadhali hizo picha kuna ‘project’ nimefanya na Stan Bakora kwa hiyo naomba zisitumike kunichafua maana mimi kuna ishu muhimu sana natarajia kuifanya kipindi hiki cha uchaguzi.
BATULI STAN BAKOLA (8)Paparazi: Oke mimi nilitaka kujua hilo tu maana nimeona jinsi picha zilivyo za mahaba nikaona ni vyema kujua mantiki ya picha hizo kutoka kwako?
Batuli: Ujue hizo picha najua atakuwa kakupatia Mkude Simba na lengo lake ni kufanya promo ya muvi yake, mimi sitapenda kwa kipindi hiki nichafuke, please naomba usizitumie.
BATULI STAN BAKOLA (9)Paparazi: Hajanipa Mkude Simba. Kikubwa nilitaka kujua hizo picha umezipigia wapi?
Batuli: Nimekwambia ni filamu na sitaki zitumike kunichafua.
Paparazi: Hiyo filamu mlishuti wapi?
Batuli: Morogoro ila  mimi sikutaka kukaa kambini, nilienda kushuti na kurudi zangu Dar.
BATULI STAN BAKOLA (10)Paparazi: Nakushukuru sana.
Alipotafutwa Stan Bakora kuhusiana na picha hizo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Batuli, alisema:
“Ni muvi kaka, katika hali ya kuuvaa uhalisia ndiyo tulipiga kimahaba zaidi lakini sina uhusiano wowote na Batuli.”

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini