Wasomi vyuo vikuu wamkubali Magufuli



Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania, Christopher Ngubiagai

SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania limemwelezea mgombea wake wa urais, Dk John Magufuli kuwa ana uwezo mkubwa wa kusimamia masuala mbalimbali ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kitaifa, hivyo anafaa kupeperusha bendera ya CCM.

Katibu Mtendaji Mkuu wa shirikisho hilo, ambalo ni la wanachama wanafunzi wa CCM, Christopher Ngubiagai alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM, Ilala Dar es Salaam kuhusu uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola.

Alisema shirikisho hilo linapenda kuwataarifu wanachama na wananchi wote kuwa CCM bado ipo madhubuti na imara zaidi hasa baada ya kumpata mgombea wake Dk Magufuli maarufu kwa jina la ‘Jembe’. “Dk Magufuli ni chimbuko kubwa la mabadiliko kwa vile ni rahisi kwake kuendana na mabadiliko ya wakati,” alisema.

Kwa upande mwingine, alisema kutokana na kujitoa uanachama wa CCM na kuhamia Chadema kwa Edward Lowassa, wasomi hawako tayari kukisaliti chama kwa maslahi ya mtu mmoja.

Alimnukuu Nyerere katika kitabu chake ‘Uhuru na Ujamaa’ 1968 katika ukurasa wa 33, alisema “Kila kizazi kina changamoto zake na kila kizazi kinapaswa kutumia fursa walizonazo kujiletea maendeleo na kufanya maisha bora”.

Alisisitiza kizazi cha sasa ni cha vijana, ambao wana nguvu, afya na mitazamo chanya na siyo wa aina ya kiongozi mwenye uchu wa madaraka na kukataa kukubali kuwa bila yeye nchi inaweza kutawalika.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini