LOWASSA na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi!

Wadau Habari; juzi ilikuwa siku ya kipekee sana kwa historia ya Tanzania ambayo tuliahidiwa na tuliisikia minong'ono mingi na tetesi za kila leo juu ya kuhama chama kwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiket ya CCM ndugu, EL.

Binafsi nampongeza kwa kuitumia haki yake ya kidemocrasia na kufanya maamuzi magumu; kama mtanzania nisiyefungamana na upande wowote nimestaajabishwa sana na mambo mawili makubwa.

Mosi ni juu ya umiliki wake wa card ya CCM, EL inasemekana ana miliki card namba 15 ya Uwanachama ndani ya CCM, lakini siku ya jana alijivua uwanachama na kupewa rasmi card ya CDM, sasa bado najiuliza imekuaje kamanda huyu amejiondoa CCM na kwenda CDM lkn bado anamiliki card ya chama hicho? Maana jana sikuona akiirudisha card ya CCM ili ichanwe chanwe pale mbele ya macho yetu.

Lakini kama hiyo haitoshi bado najiuliza inawezekanaje Kiongozi mkubwa kama yeye anathubutu kutoa majibu ya hasira mbele ya Taifa hili juu ya swali la msingi ambalo lilimchafua yeye na baadhi ya Viongozi wa wizara husika.

Kwa kusema kwamba NANUKUU; "Nilipoitisha kikao cha "Government negotiation team" nikawauliza mbona nasikia huu mkataba una matatizo? Mimi nina uzoefu wa kuvunja mikataba na huu tuuvunje! Wakaomba ruhusa watoke nje kwa saa moja, baada ya hapo waliporudi wakasema wamepigiwa simu toka mamlaka ya juu mkataba usivunjwe "what else could I have done?"

Mwisho wa KUNUKUU, Sasa najiuliza hapa inawezekanaje PM umeitisha kikao cha subordinates wako alafu anatokea wa kukuambia kuwa et nimewasiliana na wakuu wamekataa hilo, nani basi mwenye kupaswa kufanya consultation na Wakuu wenzake kati ya watu hawa wawili EL kama PM au Subordinates?

Lakini pia napata shaka pale namna ambavyo swali la msingi lilivyojibiwa kwa kusema kwamba, NANUKUU; "Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika na Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.

Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani" mwisho wa KUNUKUU; Kwa uelewa wangu wa kawaida kabisa unyeti wa jambo hili haukutaka jibu la namna hii bali watanzania tungeridhishwa zaidi endapo tungepata majibu mazuri kwa kina na yenye kujitosheleza badala ya kuwa mkali kiasi ambacho inatuacha na maswali mengi kwamba ile ni namna ya kututisha na kutuziba midomo kama ambavyo ilitokea pale kwa wana habari wenzangu au ni nini hasa?

Kama hii haitoshi bado najiuliza, Je na ile hoja ya Dr.Slaa kwamba ushahidi wa jambo hili anao na yupo tayari kwenda kuthibitisha mahakamani leo hii sisi watanzania tunaibebaje hii statement kuwa naye alikuwa anabwabwaja tu au namna gani?

Lakini nathubutu kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza Dr.Slaa na wenzake wanasimama vipi Jukwaani kumnadi kwa kumtakasa mtu huyu ambaye wao walikuwa wanachangia kumchafua?

Mambo haya yananipa shida kuyapatia majibu basi nabaki kujiuliza bila mafanikio naombeni wadau mnisaidie kung'amua.
"Majibu ya hasira kwa swali la Msingi"

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini