Mastaa Wamfuata Lowassa Ukawa


nay
Staa wa Bongo fleva, Emmanuel Elibsriki, ‘Nay wa Mitego’.
NI shidaah! Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Ngoyai Lowassa (pichani) kukaribishwa katika  Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, mastaa mbalimbali Bongo wameamua na wengine kushawishiwa kumfuata wakiamini katika uwezo wake kiuongozi, Amani limenasa mpango mkakati kamili.
Chanzo makini kililieleza gazeti hili kwamba mastaa wote waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa wakati akiwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais na baadaye jina lake kukatwa kabla ya kufikishwa Kamati Kuu (CC), wameamua kuhamia Ukawa kumfuata mwanasiasa huyo aliyejiunga huko kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
TUJIUNGE NA CHANZO
“Moto huku Ukawa umewaka. Yale makundi mawili ya M4C (Movement For Change- Chadema) na 4 U Movement (Kundi la Marafiki wa Lowassa) sasa yameingia kazini. Mkakati maalum umeandaliwa kuhakikisha kila mwenye ushawishi katika jamii anafikiwa, wakiwemo wasanii wa sanaa mbalimbali.
“Wameanza na wasanii waliokuwa nyuma ya Lowassa kwa sababu wanaamini wana wafuasi wao, ambao watashawishiwa wawashawishi hao watu wao wawaunge mkono katika kuhakikisha wanaing’oa CCM madarakani,” kilisema chanzo hicho.
wemasepetuWema Sepetu.
WEMA AKARIBISHWA
Chanzo hicho kimeweka wazi kuwa licha ya wasanii kwa jumla, lakini pia mastaa wenye mvuto mkubwa kwa jamii watafuatwa wao rasmi, kama ilivyotokea majuzi ambapo mwigizaji Wema Isaac Sepetu alifuatwa na 4 U Movement (Team Lowassa) kushawishiwa kujiunga na Team Lowassa.
Wiki iliyopita Wema alitoswa katika kura za maoni za kuwania Ubunge wa Viti Maalum (UWT-CCM) Mkoa wa Singida kwa kushika nafasi ya nne, lakini akapokewa kwa kishindo katika mapokezi yaliyojaza watu jijini Dar.
“Yaani Wema hivi karibuni aliitwa na watu wa Lowassa kwenye hoteli moja maarufu jijini Dar ambapo ajenda kubwa ni yeye kuungana na Ukawa kwa vile wanaamini ana mashabiki wengi,” kilisema chanzo hicho.
HUYU HAPA WEMA
“Ni kweli, juzi nilipigiwa simu na watu waliojitambulisha kuwa ni Team Lowassa, wakasema wana mazungumzo na mimi, ilikuwa tukutane Jumanne, lakini nilikuwa na shughuli nyingine nikashindwa kwenda.
“Tulikubaliana tukutane jana, lakini sijaelewa hasa ajenda ni nini na kwa maana hiyo siwezi kusema lolote kwa sasa kama ninaenda Ukawa au la,” alisema muigizaji huyo, alipozungumza na gazeti hili.
wolper.JPGJacquiline Wolper.
WOLPER ACHOCHEA
Kana kwamba haitoshi, staa mwingine wa filamu za Kibongo, Jacqueline Walper Massawe ambaye tangu awali alijitoa muhanga kufa pamoja kisiasa na mbunge huyo wa Monduli, anatajwa kuwa kinara wa kampeni katika mitandao mbalimbali ya kijamii akiweka wazi kuwa atamfuata Lowassa popote atakapokwenda kwani ni shabiki wake mkubwa.

LUL ANAunt Lulu.
AUNTY LULU RASMI UKAWA
Ahadi kama hiyo ilitolewa pia na mwanadada Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ aliyetangaza kujiunga rasmi na Ukawa kwa sababu ya Lowassa.
KALLAJEREMIAH1Kala Jeremiah.
Mastaa wengine ambao wamemfuata Lowassa Ukawa ni pamoja na Deogratius Shija, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Kala Jeremiah, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Bahati Bukuku.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini