MAMA DIAMOND PLATINUMZ MUNGU MKUBWA!

mama diamond (1) 
M
UNGU mkubwa! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia siha ya mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye kwa sasa yupo fiti baada ya kuugua kwa muda mrefu.
mama diamond (4)Mwaka jana, mama Diamond aliripotiwa kushambuliwa na maradhi yaliyoashiria kupooza hadi kufikia hatua ya kwenda kutibiwa India kisha kurudishwa nchini akiwa bado hajapona vizuri.
Chanzo kilicho karibu na familia ya staa huyo kilieleza kuwa, ugonjwa huo ambao ulimfanya ashindwe kutembea vizuri, ulimsumbua kwa kipindi kirefu lakini kwa sasa wanamshukuru Mungu, mama huyo anaweza kutembea mwenyewe na kuendelea na shughuli zake za kila siku.
mama diamond (2)“Wee ile ilikuwa hatari, ameumwa sana jamani mama Diamond. Hadi hatua hii ambayo amefikia kwa sasa, kwa kweli tunapaswa kumshukuru sana Mungu, ameteseka vya kutosha, sasa hivi ukimuona, shavu dodo,” kilisema chanzo hicho.
Mwanahabari wetu baada ya kupenyezewa habari hiyo, hivi karibuni alitumiwa picha ya mama Diamond akiwa fiti akitembea barabarani akifanya shughuli zake za kila siku.
mama diamond (5)Jitihada za kumpata mama Diamond azungumzie uzima wake hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kutokuwa hewani lakini Diamond alipatikana na kusema yeye pamoja na bebi wake, mama kijacho, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wanamshukuru Mungu kwani sasa mama yao yuko vizuri kiafya.
mama diamond (3)“Mama ndiyo faraja yangu siku zote. Kwa kumuona hivi mzima sasa hivi, mimi na bebi wangu (Zari) tuna amani na tunamshukuru sana Mungu, mama anatembea na kufanya shughuli zake kama zamani,” alisema Diamond.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini