Ne-Yo Aeleza Kwanini Alikuwa na Hamu ya Kuonana na DIAMOND Platnumz Alipoenda Afrika Kusini!

Muimbaji wa Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo ameitaja sababu iliyomfanya atake sana kukutana na Diamond Platnumz.
Baada ya watu kusikia kuwa nilikuwa nakuja kwenye MAMAs jina pekee ambalo walikuwa wakilitaja kwangu ni Diamond Platnumz,” Ne-Yo alimwambia Vanessa Mdee kwenye interview ya MTV Base.
 
Nikasema ni lazima nikutane na huyu jamaa, nahitaji kumuona,” aliongeza.
Siku moja kabla ya tuzo hizo pia, Diamond alielezea jinsi Ne-Yo alivyomtafuta. “Wakati nazungumza na D’banj @salaam_sk alinifata na kuniambia @neyo anakutafuta anataka kukuona…” Ungependa kujua kilichofata??? Kaa karibu na TV, Radio yaani Kiufupi Media zako Soon utayaskia,” aliandika Diamond kwenye Instagram.
Ne-Yo na Diamond ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye MTV MAMA 2015.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini