Dawa mpya kwa ajili ya kutibu magonjwa ya Kuhara na Nimonia kutua Njombe

Na Gabriel Kilamlya Njombe
Viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa na wilaya mkoani Njombe wametakiwa kwenda kutumia mihadhara inayopatikana katika kutoa elimu ya magonjwa ya Kuhara na Nimonia yanayowakumba watoto wadogo Nchini.
Kauli hiyo imetolewa na kaimu katibu tawala mkoa wa Njombe bwana Gidion Mwinami kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wakati wa warsha ya siku moja inayolenga kutoa elimu kwa viongozi hao na wataalamu wa afya juu ya kwenda kuwahamasisha wahudumu wa afya katika kukabiliana na magonjwa hayo Kwa Kutumia Dawa Mpya ya Ziora.
Kupitia Warsha hiyo Mwinami amesema anategea viongozi hao watakwenda kuwa mabalozi wazuri wa kufikisha elimu hiyo kwa wataalamu wengine wa afya ambao wamekuwa wakitoa huduma za magonjwa hayo kwa watoto huku akisema takwimu zinaonesha kuwa ugonjwa wa kuhara upo kwa asilimia 32.3 ikiwa Nimonia ni asilimia 16.3.
Kwa upande wake Dokta Rukia Ali toka wizara ya afya Amesema wamebaini kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika utoaji huduma ya afya kwa watoto hao ikiwemo baadhi ya wahudumu kutokuwa na uelewa mpana namna ya kuwahudumia watoto hao katika kukabiliana na magonjwa ya Kuhara na Nimonia.

Jackson Saitabau ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Ambaye Wakati Akifunga Warsha Hiyo Amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri Kwenda Kuwasimamia Watumishi Wao Katika Idara ya Afya Ili Waweze Kutoa Vyema Huduma ya Mama na Mtoto Kwa Lengo la Kupunguza Vifo Vya Watoto Chini ya Miaka Mitano.
Ufinyu wa Bajeti,Elimu duni Kwa Wataalamu wa Afya Pamoja na Uhaba wa Dawa Kutokana na Kucheleweshwa na MSD ni Miongoni Mwa Sababu Zilizotajwa Kukwamisha Dhamira ya Kukabiliana na Nimonia na Kuhara Kwa Watoto Waliochini ya Umri wa Miaka Mitano Jambo Linasababisha Kuwepo Kwa Vifo Kwa Watoto Hao Kila Mwaka.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini