Ibada ya kuombea uchaguzi yafanyika mkoani Iringa

Viongozi wa Juu wa Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Amina Masenza wameshiriki Ibada maalum ya kuombea Taifa amani kabla na baada ya uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.


Ibada hiyo maalum imefanyika Jumamosi hii mjini Iringa katika Kanisa Kuu la Sloam njia ya Kusini na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa Kanisa hilo.



Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa walinyanyua bendera na ramani ya Taifa wakati wa sala ya kuliombea Baraka Taifa katika Ibada hiyo maalum ambapo Kuhani wa Kanisa hilo, maarufu kama Baraka za Mungu Elia amewaomba watanzania kila mmoja kwa imani yake kuomba ili Taifa lipate kiongozi aliye na Mungu ndani yake.


Katika salam zake, Mkuu wa Mkoa amesema katika wakati huu wa kampeni na Uchaguzi, wananchi wanaweza kusikia mengi na wakati mwingine yasiyofaa yanayolenga kuwapotosha lakini ni vyema wakayapuuza kwa sababu kama serikali inataka kuwasilana wananchi hufanya hivyo moja kwa moja.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa amewataka wakazi wa Iringa kutokuwa na wasawasi juu ya kutokea kwa vitendo vya uvujifu wa amani kwa maelezo kwamba jeshi lake limejipanga kikamilifu kuzuia vitendo hivyo.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini