NAPE Amshambulia LOWASSA....Asema ni Fisadi na Hakuna Kazi Aliyofanya Bila Kuiba!

Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye ametumia dakika takribani 10 kumshambulia mgombea urais kwa kiketi ya Chadema, Edward Lowassa aliyewahi kuwa kada wa chama hicho.

Nape alirusha makombora yake kwa Lowassa jana alipopewa nafasi ya kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli katika viwanja vya Samora, mjini Iringa.
Alisema Lowassa ni mwizi na fisadi na kwamba hakuna sehemu ambayo alipewa kufanya kazi katika ngazi za CCM na serikali bila kuiba.

Nape alidai kuwa Lowassa alishindwa kukaa katika chama cha Mapinduzi kwa kuwa hawezi kufugika...."Lowassa ni Kunguru,Hafugiki." Alisema Nape.


Katika hatua nyingine,Nape alidai kuwa Lowassa aliwanunua viongozi wa ngazi za juu wa UKAWA na CHADEMA ili apate nafasi ya kugombea kupitia Chadema ambayo awali ilikuwa ikimuita fisadi.
Katika maelezo yake,Nape alisema mbunge wa Iringa mjini,mchungaji Peter Msigwa ni miongoni mwa walionunuliwa na Lowassa kwa shilingi milioni 340.

Nape amekuwa akirusha makombora kwa Lowassa tangu alipotangaza uamuzi wake wa kukihama chama hicho na kujiunga CHADEMA.
Nape aliwahi kunukuliwa akisema kuwa amekuwa akipambana na Lowassa kwa miaka 12 ndani ya CCM na kwamba mziki wake anaufahamu

Hata hivyo, tangu alipoanza kampeni zake, Lowassa amekuwa kimya bila kujibu mashambulizi ya Nape na viongozi wengine wa CCM, hali inayomfanya azidi kujipatia umaarufu mkubwa zaidi wa kisiasa.

Wakati Nape akitumia muda mrefu kurusha makombora, Lowassa yeye alikuwa Jijini Tanga akifanya mkutano mkubwa wa kampeni uliolazimika kukatishwa kutokana na mafuriko ya wananchi kuzidi eneo la mkutano.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini