PICHAZ: Hivi Ndivyo Ilivyokua Kwa Mechi za Ligi Kuu Bara Sept 27 Azam FC Vs Mbeya City na Mechi ya Mkwakwani, Tanga.

Jumapili ya September 27 ni siku ambayo mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara zimeendelea kwa michezo miwili kupigwa Dar Es Salaam na mkoani Tanga. Mechi ambazo zimechezwa September 27 ni Azam FC waliwakaribisha Mbeya City kutokea Jijini Mbeya katika uwanja wao wa Azam Complex, wakati katika uwanja wa Mkwakwani Tanga African Sports walikuwa wenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara.

John Bocco akimkumbatia Kipre Tchetche baada ya kufunga goli la pili 
Mechi imemalizika kwa klabu ya Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-1, hivyo klabu ya Mbeya City inaendelea kubakika na point zake tatu baada ya kucheza mechi zake nne kushinda moja na kupoteza mechi tatu. Magoli ya Azam FC yalifungwa na Mudathir Yahaya dakika ya 11 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Salum Abubakar

Steven Mazanda akimdhibiti David Mwantika wa Azam FC
Kipindi cha pili kilianza kwa klabu ya Mbeya City kuanza kwa kuonyesha jitihada za kutaka kutafuta goli la kusawazisha ila Salum Abubakar kwa mara nyingine tena alipiga pasi kwa Kipre Tchetche dakika ya 53 na kufunga goli la pili, Mbeya City walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa Raphael Alpha dakika ya 55.
Matokeo ya mechi ya Mkwakwani 

African Sports 1 – 0 Ndanda FC

Pichaz za mechi ya Azam FC Vs Mbeya City

Kipre Tchetche katika harakati za kutafuta goli

Mashabiki wa Mbeya City


Juma Nyoso akimdhibiti Farid Musa

Steven Mazanda mwenye mpira na Kipre Tchetche

Said Ndemla wa Simba akiwa jukwaani kutazama mechi ya Azam FC na Mbeya City

Mudathir Yahaya wakati wa kushangilia goli

Baada ya kufunga goli la kwanza wachezaji wa Azam FC wakipongezana

Mudathir Yahaya akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza

Juma Kaseja wakati wa warm Up ila hakucheza mechi ya leo

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini