Hofu ya UCHAGUZI MKUU Tanzania Yambeba BELLE 9

Wasanii wengi wa Bongo wamesitisha kutoa kazi zao katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa kuhofia kuzipoteza kwa kumezwa na kampeni za siasa, lakini Belle 9 aliamua kujitosa na kutoa video yake mpya ‘Shauri Zao’ wiki iliyopita.
Belle 9 ameiambia Bongo 5 kuwa hajutii kutoa video katika kipindi hiki kwasababu kutokana na wasanii wengi kuogopa kutoa kazi zao imefanya apate nafasi ya kazi yake kuonekana zaidi ya alivyotarajia. 

“Hakuna msanii ambaye kaachia video sasa hivi ambayo ina tension kama mimi” amesema Belle 9. “pia kati ya vitu ambavyo vinaongelewa ukiongelea watu watatu ambao wanakick nipo na mimi kwa sasa hivi, ukiingia kwenye mitandao watu ambao habari zetu zipo sana saizi. Naona uwanja umekuwa wangu peke yangu sana, kuna matokeo mazuri zaidi ya nilivyokuwa nategemea.”
Belle ameongeza kuwa video ya ‘Shauri Zao’ niliyokuwekea hapo chini ndio video yake bora kati ya video zake zote alizofanya kutokana na umakini wake na wa director Hanscana aliyeifanya.

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini