SHEIKH SHARIF AZUA MAPYA YA URAIS 2015, SOMA UONE
Sheikh Shariff Matongo akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)kuhusu ndoto yake ambayo ameoteshwa kuelekea mwaka 2015. NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII,DAR. Sheikh Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri kwa mashekh mbalimbali Duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi wasipuuze ndoto hiyo. Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi. Alisema katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali na mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Sheikh alisema ndoto nyingine kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata mafanikio makubwa kwa mwaka ...