Patcho Mwamba Akanusha Kufumaniwa na Mke wa Mtu


Mwigizaji na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba amekanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
 
Akiongea na mtandao huu, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.
 
"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini